Mwanamuziki wa Kimataifa kutoka nchini Zimbabwe, Oliver Mtukudzi akiimba moja ya nyimbo zake katika Tamasha la Filamu Zanzibar (ZIFF),lililofunguliwa rasmi usiku wa kuamkia leo katika viwanja vya Ngome Kongwe,Zanzibar.
Oliver Mtukudzi akionyesha umahiri wake wa kulicharaza gitaa wakati wa Tamasha la Filamu Zanzibar (ZIFF) usiku wa kuamkia leo.
Mwanamuziki wa Muziki wa Asili nchini,Mrisho Mpoto akienda sambamba na Mkongwe Oliver Mtukudzi wakati wa Tamasha la ZIFF linaloendelea katika viwanja vya Ngome Kongwe,Zanzibar.
Mrisho Mpoto na Ismaeel wa Mjomba Band wakiimba moja ya nyimbo zao.
Vijana wa Kundi la B six wa visiwani Zanzibar wakionyesha umahiri wao wa kuchemza mbele ya umati mkubwa uliofika Ngome Kongwe kushuhudia ufunguzi wa Tamasha la Filamu Zanzibar.
Wageni kutoka kila kona ya dunia wakiwa katika Tamasha la Filamu Zanzibar.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...