Wanachama wa klabu ya mazoezi ya viungo wakishiriki zoezi la upandaji miti.

Eneo lilioathirika na uchimbwaji wa mchanga, ambapo mazingira yake yako hatarini.

Mwenyekiti wa klabu ya mazoezi ya viungo ya
Obama akiongoza upandaji miti.

Klabu ya mazoezi ya viungo ya Obama Jana ilifanya zoezi la upandaji miti katika eneo lililokuwa likichimbwa mchanga katika kijiji cha Chechele kilichopo Donge, Wilaya ya Kaskazini B, Unguja.

Upandaji miti huo ni moja kati ya shughuli za kijamii ambazo Klabu hiyo hujihusisha nazo, shughuli nyengine inazojishughulisha nazo ni pamoja usafishaji wa mazingira katika sehemu mbali mbali zikiwemo Hospitali za Unguja na Pemba,

Zoezi hili la leo la upandaji miti lilifanyika katika eneo lililohamwa kwa uchimbaji mchanga, iumekuwa ni utaratibu wa serekali kuhifadhi mazingira ya maeneo yaliyoachwa kuchimbwa mchanga kwa kuotesha miti ili kuhifadhi uharibifu zaidi wa mazingira.

Klabu ya mazoezi ya viungo ya Obama imeendesha zoezi hili kwa nia ya kuionesha jamii na serekali kwa ujumla kwamba mbali ya shughuli za mazoezi pia inajishughulisha na mambo ya kijamii kwani wafanya mazoezi ni miongoni mwa jamii.

Wito unatolewa kwa vilabu vyengine vya mchezo huo kujitokeza katika shuguli za utunzaji wa mazingira kwa manufaa ya Taifa letu.

TUYATUNZE MAZINGIRA ILI NAYO YATUTUNZE


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 19, 2011

    Mimi nawapongeza sana kwa hizo juhudi zenu, isipokuwa hilo jina mhhhhhh!

    Hivyo hakuna jina la kiongozi wa Afrika ambaye mungeweza kutumia jina lake?

    ReplyDelete
  2. mashaalah, hongereni sana Obama, munaonyesha kwa mfano. Uongozi wa shehia usimamie kuilinda miti iliyopandwa
    Mdau
    K

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...