Mwenyekiti wa kikao Afisa wa Ubalozi Amosi Msanjila akitoa mwongozo kulia Mwenyekiti wa Tanz Uk Dr John Lusingu na kushoto Said Sururu Kutoka Tawi la Tanz Uk London.

SALAM,

Jumuiya ya WaTanzania–UK chini ya Mwenyekiti wake Dr John Lusingu, ilikutana na Viongozi mbali mabali wa Jumuiya vyama, na Taasisi mbali za KiTanzania katika juhudi ya kutathmini Mkutano wa Diaspora III, na kuweka mikakati ya utekelezaji ya mipango mingine ya Kimaendeleo.


Mwenkiti wa Tanz-Uk alisisitiza umuhimu wa kujenga utamaduni wa kuunganisha nguvu katika kupanga , kufuatilia na kutekeleza mipango mbali mbali kwa ajili ya WaTanzania walioko UK , pamoja na mikakati ya kushiriki katika maendeleo Tanzania. “Nguvu za pamoja ni resource imara katika kukabiliana na changamoto ya aina yoyote. Tunatumikia WaTanzania na Taifa moja, tukishirikiana kimawazo na kimkakati, tunahakika ya kufanikisha mambo mengi kwa haraka” alisistiza mwenyekiti Dr John Lusingu.

Viongozi wengi walioitikia mwaliko wa Tanz-UK walioshiriki katika mashauriano hayo, waliipokea hoja hiyo na kuonyesha kufurahishwa na mkakati wa “nguvu ya pamoja”, na kushauri kuwa kuwe na majadiliano zaidi kuufanya mpango huo uwe madhubuti zaidi.
Mkutano huu ulifanyika Jumamosi tarehe 18.02.11 katika ofisi zetu za Ubalozi jijini London
Asanteni
URBAN PULSE CREATIVE

kushoto Bwana Hussein kutoka tawi la TA Reading, Susan katibu mkuu wa CCM Uk na Allan kalinga Mipango, Uchumi na Fedha CCM Uk wakifuatilia agenda ya mkutano.
wajumbe kutoka ZAWA wakisiliza hoja.
Mjumbe wa Tanz Uk tawi la London Jestina akitoa hoja.
Afisa wa Ubalozi ambaye pia ni mhasibu wa Ubalozi David akichangia hoja wakati wa mkutano.
Mr Otieno (katikati) akiteta jambo na wajumbe wa TA Magabe (kushoto) na Evans (kulia) .
mwenyekiti wa Tanz Uk Dr John Lusingu akitoa mada
Picha ya pamoja baad ya mkutano.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 21, 2011

    Je TANZ-UK inaweza kutoa msaada wa kisheria kama vile "Solicitor" kwa mtanzania mwenye kuhitaji?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 21, 2011

    Kwa Vikao na Sherehe tu, hamjambo. Kila la kheri.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...