Mmoja kati ya wanafunzi 50 wa chuo cha IFM wanaochukua Bsc IT,Tumainiely Mbwambo akichora mchoro wa Kompyuta wakati wakitoa mafunzo kwa wanafunzi wa darasa la saba katika shule ya msingi Bunge iliopo katikati ya jiji leo.Wanafunzi hao wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) wameamua kujitolea kutoka mafunzo ya Kompyuta kwa vitendo kwa wanafunzi wa shule mbali mbali za msingi za jijini Dar,lengo likiwa ni kuwawezesha kufahamu kiundani kifaa hicho pamoja na matumizi yake.
 Maswali na Majibu yakiendelea kuhusiana na matumizi ya Kompyuta.
 Mwanafunzi wa IFM anaesomea masomo ya Bsc IT,Annuary Issah akitoa maelekezo ya matumizi ya Kompyuta kwa wanafunzi wa darasa la saba katika shule ya msingi Bunge leo walipofika shuleni hapo na kuanza kutoa mafunzo hayo.
 Tumaini Anderson wa IFM (kati) akiwaonyesha wanafunzi wa shule ya msingi Bunge lamna ya matumi kichapisha maandishi (keybord) ikiwa ni sehemu ya kujitolea kutoa mafunzo ya Kompyuta kwa wanafunzi wa shule za msingi za jijini Dar.
Baadhi ya Wanafunzi wa darasa la saba katika shule ya msingi Bunge,jijini Dar wakisikiliza kwa makini mafunzo ya Teknohama.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 16, 2011

    mmmmh kwani bado haipo kwenye mtaala?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 16, 2011

    This is wonderful and should be supported by all possible means. Keep up the good work guys.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 16, 2011

    Conglatulation students of IFM, Keep it up!!!

    ReplyDelete
  4. Teknohama ipo kwenye mtaala, ila hakuna waalimu wenye uwezo wa kuufundisha.

    Congratulations to IFM's students and management for this superb initiative! I look forward to seeing emulated widely and freely by other institutions of higher learning, but I hope there'll be some harmonisation on qualitative standards.

    ReplyDelete
  5. God Bless You Guys, watanzania wote tukiwa na akili na moyo wa ubunifu na kujitolea kama hawa vijana wa IFM, basi naamini kabisa kuwa tunaweza kujikwamua...

    ReplyDelete
  6. Awesome, nimeipenda hii initiative. Ni ya kuigwa

    ReplyDelete
  7. AnonymousJune 17, 2011

    Hongereni sana wanafunzi wa IFM. Ni jambo la kuigwa kwa kuwa mara nyingi tunaona wanafunzi wakiwa katika migomo si katika shughuli ya kulijenga taifa lao kama hivi. Very positive and impressive move. Keep it up guys.

    ReplyDelete
  8. Hongereni sana wadau. MUNGU awabariki. Naomba msiishie hapo, ombeni management iwaombee kwa wizara ya elimu na wizara ya sayansi na tech au wizara ya fedha wawape funds japo kidogo ili mkafundishe na mikoani mara moja moja wakati wa likizo zenu. Hali ni mbaya sana kule.Watoto hawajasoma somo hilo na walimu hawajafundishwa kulifundisha somo hilo japo liko kwenye mtaala na soon watatahiniwa kitaifa!...

    ReplyDelete
  9. AnonymousJune 17, 2011

    Kama kuna kitu cha kizalendo nimekipenda - ni hiki hapa - BIG UP IFM, sio kugoma na kuandamana tu!!!!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJune 17, 2011

    Hi guys,kip it up.i wish i could be there.
    Tumainiel, Anuary,Tumaini n mony more mmetuwakilisha sana vijana.Next tym twende shule zilizo pembezoni mwa jiji.

    ReplyDelete
  11. Thanks kwa wadau wote ambao mmeguswa kwa namna moja au njyingne katika harakati zetu za kuwafumbua wadogo zetu kuhusu somo la teknohama,hiyo ni mwanzo tu changamoto nyingi lakini hatutorudi nyuma,pamoja katika kujenga taifa imara na dhabiti,,,Annuary Issah

    ReplyDelete
  12. AnonymousJune 17, 2011

    This is awesome, Big up guyz kwa kujitolea na mungu awape nguvu zaidi msiishie hapo. This is the great idea.

    ReplyDelete
  13. AnonymousJune 18, 2011

    Hehehe shule yangu ya zamani still looking the same na madawati ni yale yale tuliyokalia miaka 25 iliyopita. Naomba wadau wote mliopitia Bunge Primary School enzi hizo mjitokeze tuisaidie shule yetu. Wengi wetu tupo wkenye position nzuri sana za kusaidia. Hii shule imetufundisha vizuri sana. Naomba kuwasilisha hii mada kwa Wadau wote wa Bunge.

    ReplyDelete
  14. AnonymousJune 18, 2011

    MUNGU awabariki kwa moyo huo wote waliojitolea ...tuwe na moyo huu watanzania..kwa manufaa ya nchi yetu sio kila kitu mpaka wazungu waje.... mdumu wadau wa kujitolea

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...