kikundi cha ngoma cha nchini rwanda kikitumbuiza katika uzinduzi wa tamasha la East Afrika Cup mkoani Kilimanjaro.
Mkurugenzi wa Michezo wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Leonard Tadeo (kushoto) akiwa katika meza kuu na viongozi wengine.
kikundi cha Tanzania waliovaa chui chui wakitumbuiza katika uwanja wa Shule ya sekondari ya moshi teki katika uzinduzi wa mashindano hayo yaliyofunguliwa leo.

Na Woinde Shizza, Kilimanjaro.

Mkurugenzi wa Michezo wa Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo, Leonard Tadeo amewataka wadau wa michezo kuhamasisha vijana wa kike wenye umri mdogo kushiriki kwenye michezo ya aina mbalimbali ili kuweza kuwajengea ujasiri, kujiamini na ushirikiano.

Amesema mbinu hiyo itasaidia serikali na jamii kwa ujumla katika harakati za kukabiliana na changamoto ya kuongezeka kwa vitendo vya unyanayasaji wa kijinsia katika jamii.

Ametoa kauli hiyo wakati akifungua tamasha la tisa la michezo kwa vijana kutoka kwenye nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki maarufu kama ‘East Africa Cup 2011’.

Tadeo alibainisha kuwa uzoefu unaonesha kwamba hali ya unyananasaji hasa kwa watoto wa kike kwenye jamii imeendelea kuongezeka katika nchi mbalimbali zikiwemo zinazounda Jumuia ya Afrika Mashariki na kushauri kuwa hatua ya vijana kushiriki kwenye michezo ni mbinu muhimu ya kuwawezesha kujenga ujuzi na kufanya wajibu wao katika jamii.

“Kwa kuwa tamasha hili la michezo linatafsiriwa kwamba ni zaidi ya kuwapa vijana fursa ya kujenga vipaji vya michezo kwa kushindanisha timu za michezo ya soka na wavu pia linawawezesha washiriki kupata elimu ya ujuzi wa masuala mbalimbali muhimu ikiwemo kubadilishana tamaduni zao ni vema fursa hiyo ikatumika kujenga jamii mpya yenye kushamini umoja na mshikamano ili kupunguza unyanyasaji wa kijinsia”alisema.

Awali akizungumza katika ufunguzi huo mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya East Africa Cup(EAC) Svein Olson alihimiza washiriki na wadau wengine wa michezo katika nchi shiriki kuendelea kuandaa vijana kuwa viongozi bora wa baadae katika jamii.

"Tamasha hili la michezo ni zaidi ya soka kwasababu pamoja na timu kushindana uwanjani lakini kupitia kusanyiko hilo vijana wanapata nafasi ya kufahamiana, kusaidiana, kujenga ujuzi, upendo na umoja utakaowawezesha kutimiza wajibu wao kwenye jamii ili kuharakisha maendeleo",alisema.

Hadi jana jioni tayari timu 96 zilikuwa zimemewasili kutoka nchi za Zambia, Zimbabwe, Kenya, Uganda, Sudani Kaskazini, Rwanda, Burundi, Zanzibar na wenyeji Tanzania.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...