Watuhumiwa wa wizi wa Pikipiki wakishikiriwa na Polisi wa Mkoa wa Morogoro baada ya kukamatwa leo  asubihi eneo la Chamwino, Manispaa ya Morogoro.
 Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Adolfina Chialo ( wa nne kutoka kushoto) akiangalia Pikipiki iliyoibiwa na kukamatwa ikiwa imefunguliwa vifaa vyake kwa lengo la kuuzwa kama vipuri , vitu kadhaa vilikamatwa vikiwemo visu kutoka kwa watuhumiwa watatu walioshikiliwa na Polisi
Watuhumiwa watatu wa wizi wa Pikipiki wakiwa chini ya Ulinzi wa Polisi baada ya kukamatwa jana eneo la Chamwino, Manispaa ya Morogoro, waliosimama ni Maofisa wa Polisi wa Mkoa akiwemo RPC, Adolfina Chialo ( mwenye sare) kabla ya watuhumiwa hao kuhojiwa. Picha na John Nditi wa Globu ya Jamii, Morogoro

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 06, 2011

    hivi nyie polisi hamuoni aibu na nyie kuuza sura hapo? hiyo sheria ya wapi?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 07, 2011

    Hao wametuhumiwa kuwa ni wizi na mtuhumiwa yeyote anakuwa hajavunja sheria mpaka imethibitishwa mbele ya mahakama na mahakama imeona amevunja sheria na kumuhukumu hapo ndipo mtuhumiwa amekuwa amethibitishwa amevunja sheria. Hakuna haki kwa polisi kuwatangaza kwenye vyombo vya habari kama ni wahalifu bila ya kupelekwa mahakamani. Sasa ikiwa hawa jamaa wakaonekana hawana hatia mahakamani na mahakama ikawaachia huru basi hapo wanao haki ya kuwashitaki hao polisi. Hapa ninachotaka kusema Polisi hawana haki ya kumtangaza mtu bila ya kupatikana na hatia na kuhukumiwa na Mahakama.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 07, 2011

    ama kweli tanzania tambarare! yaani kukamata wizi watatu tu imechukuwa zaidi ya maofisa polisi ishirini?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJune 07, 2011

    bahati yao.., polisi wangechelewa tu tungewamaliza.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJune 07, 2011

    Cheki huyo jamaa na liseni pleti kifuani! Bahati yao, zamani wangeuawawa hapo hapo na wananchi wenye hasira halafu polisi wangesema Asante kwa kutupunguzia kazi!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...