Mcheza shoo Mkongwe nchini,Aisha Madinda.
 Na Mwandishi Wetu.

MCHEZA shoo mkongwe na maarufu wa Bendi ya Muziki wa dansi ya Twanga Pepeta, Aisha Madinda leo amejiunga rasmi na Bendi ya jirani ya Extra Bongo.

Akimtambulisha kwa waandishi wa habari,Mkurugenzi wa Extra Bongo, Ally Chocky alisema anafuraha sana kumpata mcheza shoo ambaye anamini ataleta mabadiliko ndani ya Extra Bongo kulingana na uwezo wake na  jinsi anavyomfahamu.

Akizungumza na waandishi wa habari,Aisha Madinda amesema ameamua kuungana na wacheza shoo ambao anaamini akiwa nao katika safu hiyo atafanya vizuri na kipaji chake kitazidi kupanda juu zaidi.

Mkurugenzi wa Bendi ya Exta Bongo,Ally Choki akimtambulisha Aisha Madinda leo
Aisha tayari ameshaanza mazoezi na atatambulishwa rasmi kwa mashabiki jumatno kwenye Klabu ya masai Ilala jijini Dar es Salaam

Kiongozi wa wacheza Shoo, Super Nyamwela alimkaribisha Aisha kwa mikono miwili na kusema sasa kazi imekamilika na kuwataka wapenzi na mashabiki wajitokeze kwa wingi mara ya kwanza wanapomtambulisha Aisha pale klabu masai Ilala ndipo moto mkali wa Exra Bongo utaanza kuwaka

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 18, 2011

    ZE FULANAZ ILIPIGWA PHOTOCOY NINI NA ALLY CHOKI NDIO IMETOKA RANGI HIYO EH?????? SI ILE YA SKY BLUE NA WEUPE??? YA ANKAL MICHUZI.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 19, 2011

    mi naona kesha kuwa mtu mzima shughuli haziwezi tena, ni bora angekaa nyumbani tu akawachia vijana sasa

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...