Hi Michuzi
 
Naomba uwatolee wadau kwenye blog ya jamii picha hizo. Swali langu ni kwamba je hizi ndizo zilikuwa bendera za Tanganyika kwa wakati huo?  Na kwa nini kuna ya blue na kuna nyekundu? Mwenye historia naomba atufahamishe.
 
Mdau Mkiramweni

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 04, 2011

    MH! naombeni msaada wenu wadau, Hivi bendera ikiwa na rangi nyekundu si inamaana hiyo nchi ilimwaga dmu? au historia niliyosoma ilikuwa si ya kweli? sasa kama ni hivyo iweje tanzania tuwe na bendera yernye rangi nyekundu wakati hatukumwaga damu?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 04, 2011

    Anony wa kwanza labda ungeelewa kwamba mdau aliuliza swali kama hizo ndizo bendera za Tanganyika kabla ya uhuru? Tofautisha pia Tanganyika na Tanzania.

    Mimi ninvyoona kama hizo ndizo zilizokuwa bendera za wakati zilikuwa zinawakilisha wakoloni waliotutawala na sio mambo ya kumwaga damu au kutomwaga damu. Hizo bendera mkiziangalia zinawakalisha Uingerza ambayo bdiyo nchi iliyotawala tanzania katika kipindi cha 1919......19961.

    lakini nikirudi kwenye historia yako bado naona hata bendera ya sasa ya Tanzania bado ingepaswa iwe na rangi nyekundu kwa sababu damu ilimwagika wakati wa mkoloni. Kumbuka vita ya MajiMaji. Wajerumani waliua watanzania (watanganyika kwa wakati huo) wapatao laki tatu. Uwakumbuke pia na akina Mtemi Mkwawa na wengine wengi waliopoteza maisha yao wakati wa ukoloni. Na hata kama tumeungana na zanzibar, bado rangi nyekundu ingetakiwa kwani Zanzibar walimwaga damu katika mapinduzi. Je hawa hawawezi kujumuishwa katika watu waliopigania uhuru wa nchi yetu? Kwa hiyo kama historia yako ni ya kweli, basi bendera ya Tanzania ilitakiwa iwe na rangi nyekundu.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 04, 2011

    Tulimwaga damu sana Tanzania na Zanzibar. Lakini tumeshauriwa tusijikumbushe hayo yamepita ili tuishi kwa amani na tupate misaada.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 04, 2011

    Sio lazima sababu kumemwagika maji ndio iwe Nyekundu lazima kusahau Mabaya jamani Mandela aliwafanya wazungu wajinga kwa kuwapuuzia umeona limewaumiza makosa yao.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 04, 2011

    http://www.britishpathe.com/

    Hiyo Website hapo juu andikeni Tanganyika au Zanzibar mtaona enzi za uhuru na kabla ya uhuru Tanzania na pia ufisadi wa UK waliufanya kujifanya wanatengeneza Barabara kumbe wanaiba mazao ya Karanga kuuza nje ndio kipindi hiko ilikuwa bishara kubwa UFISADI tumerisi na Tabia hata za michezo tumerisi WAENGEREZA bora hata tungerisi WAJERUMANI tusingekuwa wavivu. MZ

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 04, 2011

    Mimi nadhani bendera hizi zirejeshwe na hasa ile nyekundu pili muungano wetu utakapotambua kuwa umuhimu wa kuwepo bendera ya Tanganyika kwaajili ya serikali ya Tanganyika.

    Wanablogu lazima watambue mfano mdoogo wa Muungano, siku zote kwakutumia uzoefu wa mahusiano, muungano una matokeo yafuatayo;

    1. Muungano wa vitu viwili kuzaa kimoja an kuwa kitu kimoja ( Kuunganika)

    2. Muungano wa vitu viwili kuzaa kitu cha tatu, ikiwa kile cha tatu ndicho kinaelezea na kuleta maana ya kuwa wana mtizamo wa kitu kimoja na uchungu sawa kwa kile kimoja mfano, katika ndoa ya watu wawili kuzaa watoto, ikiwa watoto ndio kiungo cha wale wawili.

    Mwisho umuhimu wa kuwepo Tanganyika ni mkubwa maana ni kama ndoa iliyoondokewa na mwanandoa mmoja, ambaye ni Tanganyika na bendera yake nyekundu na twiga katikati.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 04, 2011

    Wadau mi najua hiyo nyekundu ndio haswaa ilikua bendera ya mkoloni kati ya mwaka 1919 - 1961, ila hiyo ya bluu sina uhakika nayo na wala sina taarifa zake za kutosha.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...