Wachezaji wa timu mchanganyiko wa mabenki yalioopo visiwani Zanzibar wakifurahia baada ya kunyakua kombe kwa kuwasambaratisha Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa mabao 6-5 yaliyopatikana kwa mikwaju ya penati kwenye mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Mao Tse Tung mjini Zanzibar,ikiwa ni Bonanza la michezo kwa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Wafanyakazi wa Mabenki yaliyopo Visiwani humo..
Mchezaji wa timu ya benki Mohamed Himid (kushoto) akiwania mpira na Hassan Hamad wa timu ya Baraza la Wawakilishi kwenye mchezo wa kusisimua uliofanyika jana kwenye uwanja wa Mao Tse Tung mjini Zanzibar.Timu ya Benki ilipata ushindi wa Penati 6-5 baada ya kutoka sare ya 2-2 katika muda wa kawaida.
Naibu Waziri wa Afya na Utibabu, Dk.Sira Ubwa Mamboya (wa pili kulia) akichuana na akina mama kutoka timu mchanganyiko ya mabenki kwenye mchezo wa kufukuza kuku ambao mwana mama kutoka timu ya benki alifanikiwa kumnyakua kuku huyo.Picha na Mdau Martin Kabemba.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 18, 2011

    Kwa kweli kuku amenimaliza jinsi alivyowakatisha kona isiyotegemewa hao washiriki!

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 18, 2011

    kutesa wanyama tu halafu analiwa..... chezeni rede

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...