Bw. David Jairo
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo amepewa likizo ili  kupisha uchunguzi juu ya tuhuma zinazomkabili kupata ukweli kabla ya kuendelea na hatua nyingine juu yake . 

Katibu Mkuu Kiongozi, Bw. Phillemon Luhanjo alisema yeye akiwa ndiye mwenye mamlaka ya
nidhamu, kwa kuwa tuhuma zinazomhusu Jairo zinahusu fedha, amemteua Mkaguzi na
Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na kumpa siku 10 afanye uchunguzi wa
awali.
Luhanjo alisema ndani ya siku kati ya mbili na tatu atakuwa amemteua Kaimu wa
nafasi hiyo wakati Jairo akiwa likizo ya malipo. “Siku mbili, tatu mtasikia nani
nimemteua,” alisema Luhanjo.

Katibu Mkuu alitoa taarifa hiyo leo mjini Dodoma kwa waandishi wa habari na
kuzitaja tuhuma zinazomhusu Jairo kuwa ni nzito hali ambayo imemlazimu kuamua
aende likizo licha ya kwamba Sheria Na. 8 ya mwaka 2002 na kanuni zake za
utumishi wa umma 2003, inaruhusu mtuhumiwa kuruhusiwa kuendelea na kazi wakati
uchunguzi ukifanywa. 

Kwa mujibu wa Luhanjo, tuhuma zinazochunguzwa zilizotolewa na baadhi ya wabunge
wakati wakichangia hotuba, walimtuhumu Jairo kuhusika na tuhuma mbalimbali ikiwamo ya kuzitaka taasisi, vitengo na idara zilizo chini ya Wizara zichangie Sh milioni 50 kila moja ili fedha hizo zitumike kuwalipa wabunge kufanikisha mawasiliano ya bajeti.
 
Tuhuma nyingine ni za kuwalipa masurufu ya safari watumishi walio chini ya
Wizara na Taasisi zake ambao tayari walishalipwa na wizara na taasisi zao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 22, 2011

    Hii pesa ya kuchakachua kweli haitoshi,maana jamaa angeachia tu ngazi akapata mda wa kuwa karibu na familia na kula pesa aliyojilimbikizia yeye na familia yake kutoka kwa walipa kodi wasio na umeme , maji, wala milo 3.
    Hivi huoni kuwa ni raha sana kujiuzuru na kuinjoi maisha yaliyobaki?au ndio mpaka muadhirike mkiwa kwenye madaraka?
    Umeshaharibu ng'amuka na wengine waendelee,kuna vijana wengi wamemaliza vyuo kazi hawana ,sasa mnang'ang'ania madaraka mpaka lini?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 22, 2011

    Tunawatakia uchunguzi mwema, ila kwa hili wabunge waliharakisha kidogo na pengine wanaweza kuumbuka. Tusiwe wepesi wa ku-judge badala ya kupata facts zote na wabunge wanatengeneza Taifa la walalamishi badala ya kuhimiza watu kufanya kazi kujenga nchi.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 22, 2011

    Ustaadhi umebania maoni yangu:
    Narudia tena huyu jamaa pesa aliyojilimbikizia inamtosha yeye na vizazi vyake si ajiuzuru tu na awaachie wengine na yeye akamalizie uhai wake kuwa karibu na familia yake.
    Walipa kodi wanataabika katika nchi yao kwa sababu ya hawa watu.Kila leo ni uchakachuaji tu,hakuna audilifu wala ufanisi.
    Vijana wengi wanamaliza vyuoni kazi hawana,kazi zimekaliwa na hawa wazee miaka nenda miaka rudi ,je kutakuwa na maendeleo hapo?

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 22, 2011

    hivi ndivyo inatakiwa. kama kuna tuhuma zozote juu ya mtu nchi nyingi huyo mtu ata step aside halafu investigations zinafanywa na kama akikutwa na hatia sheria inachukua mkondo wake eg anaachishwa kazi au anafunguliwa kesi. akikutwa hana hatia anarudishwa kazini.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 22, 2011

    Hiki ni kiini macho tu.huu ni mchezo wa wizara zote tatizo ni huyo Masebu kaamua kwamba SASA BAAAAAAAAAAAAAAAAAS.lakini wabunge waanavutaga sana.duh....nchi hii

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 22, 2011

    Hivi wewe unaesema wabunge wameharakisha wanaweza kuumbuka we ndio huna akili kabisaaaaaaaa,mtu anachakachua kila mtu kajua ajiuzulu tuu tunateseka umeme shida maji nayo yameanza kuwa shida yani hii serikali basi tuu ila mwisho wenu utafika mnachukua kodi zetu mnazitafuna tuu kila wakati haiwezekani 2015 hapa patakuwa hapatoshi tumechokaaaaaa kila siku yanazuka mapya kuiba fedha si mtafute utafiti tupate UMEME au kwasababu nyie viongozi hampati kero tunayopata wananchi ole wenu 2015 .

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 22, 2011

    Kwa kweli hatua iliyochukuliwa dhidi yake ni sawa kabisa. Uchunguzi ufanyike na ukweli utapatikana na hatua zitachukuliwa kwa usalama na haki.Mungu ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  8. Kwanza nimshukuru mno Mtukufu Rais kwa kujali natural justice, pili nikuombe kaka yangu David usitie hofu yoyote mwenyezi Mungu yu pamoja nawe kwani fitna za akina shelukindo hazitakunyima haki yako. Uchunguzi wote ni mzuri, wa kwanza uko wazi kabisa kwani waraka ulikuwa wa wazi na fedha zimeingizwa akaunti ya Taasisi. Sasa tuache vyombo vilivyopewa dhamana ya kufanya uchunguzi vifanye kazi yake na ndipo tutajua mbivu na mbichi

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 22, 2011

    hiyo kesi ni ya ngedere kwa nyani! barua yake inasema hivi, nanukuu"Kama ilivyo kawaida yetu wakati wa bajeti........"kwa mantiki hiyo,ni jambo ambalo ni endelevu kuchangishana.hapa tuone kosa ni kwa nini barua ilimfikia mbunge shelukindo,na walipa kodi wakalijua hili.kuvujisha siri ndo chanjo haswa cha kosa.otherwise ni maswala ya kiufundi yanayofanyika wakati wa bajet.hiyo likizo ni danganya toto na atarud kazin kweupe,akae bench kidogo,watu wapunguze ngebe.wabunge wengine si unajua hawajui kinachoendelea nchi hii mpaka wakae kwenye kamati wapewe mabahasha mazito!!!!

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 22, 2011

    Hapa Mhe. Shellukindo popote ulipo ujue kuwa waliokutengeneza wamekuwashia moto, fedha zinaingizwa kwenye taasisi ya Serikali na si akaunti ya mtu binafsi kwa hiyo ni rahisi sana kujua zilipokwenda, na mchangiaji uliyonukuu "Kama iliyo kawaida yetu wakati wa bajeti...." hujamalizia sentensi nzima, hiyo inasema kawaida ya maafisa waandamizi kuambatana na viongozi wa Wizara, hivi jamani wengi wetu tumesoma kweli? hapo suala ya rushwa liko mbali sana na maelezo yaliyoko kwenye barua. Kumbuka watu wanaweza kukufanyia fitina hata wewe unashabikia Jairo afukuzwe. Kwenye masuala ya kazi kuna fitina na chuki na hilo liko wazi. NB. Tafadhali tunaomba kujua na Mhe. amepata wapi barua ya Serikali, watu wa usalama watatusaidia kwa hili.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 22, 2011

    hivi katibu anaweza kuamua yote hayo bila idhini ya waziri husika?we unaesema zinaingia serikali akili yako ina wadudu!!We nahisi ulihongwa shati ndo maana hata uelewi unaongea nn!!


    Mdau ugaibuni

    ReplyDelete
  12. AnonymousJuly 22, 2011

    Sipendi rushwa na nachukia rushwa lakini ili la Bwana Jairo liko wazi. Sioni rushwa imetoka wapi. Barua inajieleza kuwa kwamba watumishi watakuwa Dodoma na wanalipwa posho na cashier au mhasibu hawezi kubeba fedha zote mfukoni lazima ziingie kwenye taasisi mojawapo ya Wizara na ndicho kilichofanyika. Of course pesa kama itakuwa imeingizwa siyo lazima itumike yote pili kuna huu utamaduni kwamba Wizara ikishapitisha budget yake lazima watu kidogo wapate ka-sherehe kidogo, sasa unadhani pesa itatoka wapi. Ni wapi ambako baada ya kufanikisha kazi hawasherekei?
    Tatu huyu mama ana document ya serikali ambayo ni siri je siyo kosa la jinai, anaweza kueleza ameipataje. Kuwa na document kama hiyo lazima either upate kibali toka mahakamani au kwa njia yoyote halali. Je serikali iko tayari kumchukulia hatua kuiba nyaraka za serikali?

    ReplyDelete
  13. AnonymousJuly 22, 2011

    Nawashangaa mnaomtetea. Je hamjui kuwa hizo fedha si kuwa ziliingia tu bali zilitoka. Zilipelekwa wapi? Na nani amempa mamlaka ya kufanya harambee ya billion? Kwa idhini ya nani kaamua kutumia billioni nzima? Je budget iliyopita aliiomba hiyo ela? How can someone raise a billion from government offices and say that he is innocent? How much do they misuse under the carpet and mind you its our money. Mimi nalipa tax mpaka nasikia maumivu almost half of my salary inaenda kwenye kodi wanazotumbua hawa walafi!

    ReplyDelete
  14. AnonymousJuly 22, 2011

    siku 10 kwa uchunguzi wa awali, halafu miezi kadhaa kuunda kamati ya kuchunguza kwa undani, kisha mwaka na ushee kamati kufikisha ripoti bungeni, inafuatia na miezi miwili na nusu kwa spika na kamati yake kuzingatia ripoti iliyofikishwa kwake, kabla ya yeye spika kuandika ripoti yake kwenda kwa rais. Ifikapo kwa rais tayari ni wakati wa uchaguzi mkuu, kesi inawekwa upande ili watu watie nguvu zote katika kampeni za uchaguzi. Baada ya miezi minane ya kampeni CCM inashinda na watanzania tushasahau yaliopita miaka mitatu na ushee nyuma.

    ReplyDelete
  15. AnonymousJuly 22, 2011

    Mdau wa Ughaibuni, Acha Jazba. Hiyo Barua ni Barua ya wazi na sio ya Kificho. Fedha zimeingizwa katika Account ya GST ambayo iko chini ya wizara ya Nishati na Madini, na sio NGO ya Jairo. Na hicho ndicho anachosema mdau unayemtukana. Inaeleweka kwamba mlolongo mzima ni wa kifisadi, lakini kwa ushahidi uliopo huwezi kumfunga Jairo. Tatizo, ni nani wa kuwakamata hao wabunge wanaopokea mibahasha yake ili kupitisha Bajeti? Na hiyo fedha hutolewa kwa njia gani kutoka katika account ya serikali (GST in this case) kwenda kwa Wabunge? Je zilikwishatolewa au bado? Kama bado, ndiyo maana mdau mmoja anasema hili suala limeharakishwa, maana utamkamata nani hapo na kwa tuhuma zipi?

    ReplyDelete
  16. AnonymousJuly 22, 2011

    Huyo naye eti Taifa la walalamishi, we umetokea Libya au Somalia. Tuna haki ya kulalamika kwani uonevu umezidi kama hujui au huoni kilio chetu just keep quite, au wamekutuma? Mi naona hapo tu kuna kamchezo likizo ya malipo kwa mwizi, muongo!!!!!! Hivi jamani si watusaidie basi hata umeme tu tujue wanaakili. Ila mwenye shibe hamjui mwenye njaa maana umeme ukikatika kwa wakubwa upo, so nyie subirini hasira mnayoichochea kwetu mtajuta na mdau usinibanie waache wasome tumewachoka na wala si uongo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...