Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk.Hussein Mwinyi akizindua Kitabu cha dini cha Mwezi Upi Sahihi wa ‘Kitaifa’ au wa ‘Kimataifa’. Kushoto ni mtunzi wa Kitabu hicho, Sheikh Profesa Mikidadi Juma na Mwenyekiti wa jopo la masheikh na wanazuoni wa Kiislamu Tanzania, Sheikh Sharif Hassan Hashim. Hafla hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk.Hussein Mwinyi akizungumza wakati wa uzindua wa Kitabu cha dini cha Mwezi Upi Sahihi wa ‘Kitaifa’ au wa ‘Kimataifa’. Kushoto ni mtunzi wa Kitabu hicho, Sheikh Mikidadi Juma na wa pili kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa jopo la masheikh na wanazuoni wa Kiislamu Tanzania, Sheikh Sharif Hassan Hashim. Hafla hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam.
 Bango la uzinduzi
 Mawaidha yakitolewa wakati wa uzinduzi huo
Sehemu ya waliohudhuria hafla hiyo adhimu. Picha na Francis Dande wa Globu ya Jamii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 18, 2011

    Mwezi Mtukufu wa Ramadhani hauko mbali, Mwenyezi Mungu ajaalie tofauti za kuanza kufunga na kufungua zisitokee tena.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 18, 2011

    hii jumuia si ingelikuwa murua zaidi kama ingelikuwa na jina la kiswahili na kiarabu badala ya kiswahili na kiingilishi? Hasa ukitilia maanani ni jumuia ya kiislamu na lugha kuu pamoja na maamrisho ya dini hii yako katika kiarabu?

    ReplyDelete
  3. Hivi kuna miezi mingapi? hili kwangu naona linawachanganya waumini, ingetakiwa maulamaa, wake pamoja wakubaliane, na waondoe tofauti zao, au wawaweke waumini sawa, kuwakutokana na hili na lile ni hiayari yako sasa kufuata huu au ule, kama ipo hivyo!

    ReplyDelete
  4. Utandawazi umekua, na hii ni sehemu ya changamoto inayokabili Waislamu katika masuala mfano wa haya. Leo hii mtu akitazama channel za Uarabuni mfano wa Saudia au Peace TV, anaona watu wakiswali swala mathalan taraaweh katika wakati ule ule na tarehe ile ile ya hapa kwetu. Utamlaumu mtu kwa hili, hasa ukizingatia kuwa mwezi ni mmoja tu duniani?

    ReplyDelete
  5. nahitaji hiki kitabu mwenye kujua namna ya kukipata

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...