Na Mwandishi Wetu
BENKI ya Exim imesema itaendelea kuweka nguvu kusaidia mambo mbalimbali ya kijamii ikiwemo michezo katika bajeti zao za kila mwaka kama mojawapo ya majukumu yake mbali na yale ya kibenki.

Meneja Masoko na Uhusiano wa benki hiyo Linda Chiza  aliyasema hayo Dar es Salaam jana baada kumalizika kwa mashindano ya Kombe la Lamennais yaliyofanyika wilayani Babati mkoani Manyara hivi karibuni na kudhaminiwa na benki hiyo.

Mashindano hayo ya kila mwaka ya ujirani mwema yaliandaliwa na Shule ya Sekondari ya Singe na kushirikisha timu mbalimbali kutoka sekondari tofauti nchini.

Pamoja na udhamini huo kwa mashindano hayo,Chiza alizitaka sekta nyingine binafsi kuingia katika udhamini wa michezo ili kupanua wigo wa ushindani wa michezo nchini na hatimaye kupata wawakilishi wengi zaidi katika michuano ya kimataifa.

“Tuna programu maalumu za kusaidia mambo mbalimbali ya kijamii ikiwemo michezo kama moja ya majukumu yetu lakini pamoja nasi tunawaomba wadau wengine katika sekta binafsi kusaidia michezo ili kuongeza wigo wa ushindani na kupata wawakilishi wengi zaidi katika michuano ya kimataifa”,alisema Chiza.

Alisema pamoja na udhamini wa mashindano, vyama vya michezo husika vinahitaji kusaidiwa kupata vifaa vya kisasa vya michezo yao na kwamba serikali pekee haiwezi kuyafanya yote hayo hivyo kuna haja ya kipekee kwa wadau wengine kuongeza nguvu katika hilo.

“Serikali imekuwa ikijitahidi kwa kadri ya uwezo wake kuhakikisha michezo yote inakuwa katika kiwango cha kuridhisha nchini lakini bado ipo haja kwa wadau husika kuongeza nguvu ili vyama husika viweze kuwakilisha vizuri katika ngazi za kitaifa na kimataifa”, aliongeza Chiza. 

Pamoja na Singe, shule nyingine zilizoshiriki ni pamoja na St. Antony ya Dar es Salaam,Majengo ya Moshi,Duluti ya Mbeya,Uchama ya Tabora,St. Martin ya Kenya,Mpeketon ya Malindi Kenya,Kilimanjaro Boys ya Moshi, St. Martin Junior ya Meru Kenya na Mpanda Hill ya Mbeya.

Katika michuano hiyo iliyohusisha michezo ya mpira wa Miguu, Pete, Wavu na Kikapu timu za sekondari ya Singe zilichachafya wengine kwa kuibuka washindi katika michezo mitatu na sekondari ya St. Antony ikajitutumua na kushinda katika Kikapu.

Sekondari ya Mpanda Hill ilionyesha upinzani kwa kushika nafasi ya pili katika michezo ya mpira wa Miguu,Pete na Wavu huku St. Antony ikiendelea kujitutumua na kuambualia nafasi ya tatu  katika michezo hiyo.

Washindi walipatiwa kombe  na zawadi nyingine kadhaa za kimichezo ikiwemo mipira kutoka kwa benki ya Exim Tanzania waliodhamini ambapo pia timu zote shiriki zilipatiwa zawadi tofauti katika kutambua ushiriki wao.

Benki ya Exim imekuwa na mchango mkubwa katika kuinua michezo nchini ambapo pia imewahi kudhamini Wanariadha katika mashindano ya ndani na nje ya nchi pamoja na Gofu kwa nyakati tofauti.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...