Hayati Dennis Joseph Masanja
Familia ya Bw. Shabani-Kessi na Bibi Devota (Kijogoo) Mtambo wa Mbezi Beach, Dar es Salaam inapenda kuchukua nafasi hii kutoa shukrani zao za dhati kwa ndugu, jamaa, marafiki, majirani na wale wote waliojumuika nao kwenye msiba wa mtoto wao mpendwa Denis Joseph Masanja uliotokea tarehe 15 Juni 2011 na mazishi yaliyofanyika tarehe 18 Juni 2011 Dar es Salaam.

Familia inashukuru kwa kupewa faraja kubwa wakati wa kipindi kigumu cha msiba wa mtoto wao mpenzi Dennis na inawaombea wote kwa Mwenyezi Mungu awajalie baraka tele.

Shukrani za pekee ziwafikie Paroko, Jumuiya na Wanakwaya wa Kanisa Katoliki la Mt. Gaspari wa Mbezi Beach, Dar es Salaam; Father Veri Mturushwe Urio wa Kanisa RC Mtakatifu Anna, Kinondoni Dar es Salaam, wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (waliopo ndani na nje ya nchi), Kampuni ya Simu Vodacom, Standard Chartered Bank na Benki kuu ya Tanzania; majirani wote ikiwa ni pamoja na Familia ya Msaki, Meja Mstaafu Fatuma Myalla, Ezra Mzirai, Peter Kajiru, Hussein Katanga, Salim Madati Kikundi Maalum cha marafiki wa Shabani-Kessi & Devota, na Walpha Tours. Kwa kuwa ni vigumu kumshukuru kila mtu mmoja mmoja, familia inatoa shukrani za pamoja kwa wote walioshiriki kwa namna moja au ingine katika kipindi chote cha maombolezi.

Familia inamshukuru Mungu kwa zawadi ya maisha aliyompatia mtoto Denis hadi siku iliyompendeza kumuita kwake. Denis atakumbukwa milele katika mioyo na mawazo na kwa imani kwamba siku moja Mungu atatukutanisha naye.

Denis, tulikupenda lakini Mwenyezi Mungu amekupenda zaidi.
Raha ya milele umpe eeh Bwana, na mwanga wa milele umwangazie. Apumzike kwa amani -  Amina.

Familia inawakaribisha wote katika Misa ya Shukrani itakayofanyika nyumbani Mbezi Beach, Jumamosi tarehe 23 Julai 2011 kuanzia saa 1.30 asubuhi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Kiondo familyJuly 21, 2011

    2 Corinthians1:3-4 What a wonderful God we have-He is the Father of our Lord Jesus Christ, the source of every mercy, and the one who so wonderfully comforts and strengthens us in our hardships and trials. And why does He doe this? So that when others are troubled, needing our sympathy and encouragement, we can pass on to them this same help and comfort God has given us.

    R.I.P. our loved one.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 21, 2011

    RIP Dennis

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 22, 2011

    I have heard that this was a brutal murder case that was very unfair to this cute young boy...RIP Denis.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 22, 2011

    RIP Dennis, always u will be remembered.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 09, 2014

    I miss you dear boy...Its so unbelievable that you are gone,june has been a sad month for me since my father joined you in heaven on June 29th

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...