Februari 1990: Marehemu Dr Omar Ali Juma, wakati huo akiwa Waziri Kiongozi wa Zanzibar,  akimpokea Mzee Nelson Mandela na mkewe Winnie Uwanja wa ndege wa Zanzibar siku chache baada ya Madiba kuachiliwa huru na kabla hajawa Rais wa kwanza Mweusi wa  Jamhuri ya Afrika ya Kusini

Leo ni miaka 10 tokea aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.Omar Ali Juma alifariki dunia ghafla nyumbani kwake jijini Dar es salaam July 4,  2001. 

Wakati wa uhai wake alishika nyadhifa mbalimbali serikalini ikiwa ni pamoja na Waziri Kiongozi wa Zanzibar toka January 25, 1988  hadi October 1995. Kutoka 1995 hadi 2001, alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Dk. Omar alizaliwa tarehe 26 Juni, 1941 katika kijiji cha Wawi, Wilaya ya Chakechake, Kusini mwa Mkoa wa Pemba.

Elimu yake ya msingi aliipata katika Shule ya Msingi ya wavulana ya Chake, ambayo kwa sasa inajulikana kama Shule ya Msingi Michakaini tangu mwaka 1949 mpaka mwaka 1957.

Elimu ya sekondari aliipata katika Shule ya Sekondari ya Euan Smith Madressa, ambayo nayo hivi sasa imebadilishwa jina na kuitwa Shule ya Sekondari ya Haile Selassie tangu mwaka 1957 hadi 1960. Kuhusu elimu ya juu aliipatia kwenye vyuo mbalimbali tofauti vilivyomo nchini Tanzania na nje.

Alianza kusoma katika Chuo Kikuu cha Moscow State, ambako alimaliza mwaka 1967 na pia mwaka 1969 alimaliza katika Chuo Kikuu cha Cairo, Misri.

Pia alisoma Chuo Kikuu cha Edimburgh ambapo napo alimaliza masomo yake mwaka 1977, akapata nafasi tena ya kwenda kusoma Chuo Kikuu cha Florida, Marekani na alimaliza mwaka 1980.

Dk. Omar aliendelea na masomo yake na mwaka 1982 alikuwa mmoja wa wahitimu katika Chuo Kikuu cha Reading, Uingereza na pia kiongozi huyu alipata fursa ya kwenda kusoma katika Chuo cha Kivukoni Ideological mwaka 1982.
[hariri]Shughili za Kiserikali

Dk. Omar Ali Juma alikuwa mfanyakazi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar tangu mwaka 1967 hadi mwaka 1984 ambapo alihamishiwa katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 1995 hadi alipofariki dunia.

Alipokuwa mfanyakazi wa Serikali ya Mapinduzi 
ya Zanzibar (SMZ) alishika nyadhifa nyingi kubwa.

Mwaka 1967 - 1969 alikuwa Ofisa Wanyama Msaidizi, mwaka 1969 - 1970 alikuwa Ofisa Wanyama na mwaka 1970 hadi 1971 alikuwa Ofisa Wanyama Mwandamizi.

Mwaka 1971 -1972 alikuwa Ofisa Mifugo, pia alikuwa Ofisa Mkuu wa Mifugo katika miaka ya 1972-1978.

Wakati mwaka 1978-1984, alifanikiwa kushika wadhifa wa Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mifugo, mwaka 1984-1987 alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo na Maendeleo ya Mifugo, Zanzibar, na Januari 1988 - 1995, alikuwa Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...