Waziri Mkuu, Mh. Mizengo Pinda na Spika wa Bunge,Mh. Anne Makinda (kushoto) wakitazama vifaa vya maabara baada ya Waziri Mkuu kuzindua Meza ya Maabara inayohamishika kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma leo.
Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma leo mara baada ya kuzindua maabara ya kutembea.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Anne Makinda akitoa changamoto kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Zanaki ya jijini Dar es Salaam na Shule ya Sekondari Dodoma kuwa wasome kwa bidii na kuepuka migomo . Wanafunzi hao walikuwa Bungeni leo ili kushuhudia bajeti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na kuangalia shughuli za Bunge.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa(katikati) akiwa na mbunge wa Jimbo la Kinondoni,Mh. Iddy Azan (kushoto) na mbunge wa jimbo la Kawe,Mh. Halima Mdee wakiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Zanaki ya jijini Dar es Salaam ambao walikuwa Bungeni leo kushuhudia bajeti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 20, 2011

    Dk.Kawambwa jitahidini sana hizo shule za serikali zirudi kwenye kiwango cha juu cha Elimu kama ilivyokuwa Zamani.Nani asiyekumbuka enzi za Mazengo,Tosamaganga,Ihungo,Kahororo,Nyakato,Umbwe,Zanaki,Weruweru,Pugu,Minaki,Ilboru,Rugambwa,Mkwawa Iringa girls,IfundaTech?,Azania,Jangwani,ShyCom,Ndanda,Tanga school,Moshi Tech,Nganza,Bwiru boys/girls,Musoma boys,Tabora boys/girls,.n.k zinapwaya sana siku hizi kwenye mitihani.Pliiz Michuzi usiibane nikumbuka mbali sana mzee wa kazi

    David V

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 20, 2011

    Jamani Mh. Halima Mdee naye ametulia kweli! Hivi ameolewa au yuko single! She is a beatiful girl! Big up mheshimiwa!!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...