Kwanza kabisa tunapenda kuupongeza uongozi wa SIMBA SPORTS CLUB (SIMBA B) kwa kukubali kucheza mchezo wa kirafiki timu yetu ya KILIMANJARO RANGERS FC katika uwanja wa Ushirika Moshi tarehe 20/07/2011 na kutufunga 4 - 1. Tumefarijika sana kwa hili. 

Japo tumepoteza mchezo huu lakini wametujengea mazingira mazuri ya uaminifu kwa timu nyingine tutakazopenda kucheza nazo na pia nichukue fursa hii kuomba viongozi wa timu nyingine kubwa za soka hapa nchini kusaidia soka la timu zinazochipukia kama za kwetu pindi wanapotuma maombi ya kucheza nao. TUNASEMA ASANTENI SANA SIMBA SPORTS CLUB kwa kukubali wito wetu.
Zaidi kwa habari zetu msisite kututembelea katika libeneke letu www.kilimanjarorangersfc.com
Naomba kuwasilisha
Mwenyekiti
Kilimanjaro Rangers FC

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...