Waziri wa Kazi na Ajira Mh. Gaudencia Kabaka akisikiliza kwa makini maelezo ya mradi wa ujenzi wa nyumba za bei nafuu kutoka kwa Mkurugenzi wa Uendeshaji Patrick Mongella jana jijini Dar es salaam. Nyumba hizo zinajegwa na Mfuko wa Pensheni kwa watumishi wa umma (PSPF). Waziri huyo na Naibu Wake Dkt Makongoro Mahanga walipata maelezo ya mradi huo wakati walipotembelea banda la Wizara ya Fedha katika maonyesho ya 35 ya kimataifa ya Dar es salaam.
Juu na chini ni baadhi ya wanafunzi wa kidato cha tano na sita kutoka Shule ya Sekondari ya Morogoro walipata maelezo mafupi kuhusu historia ya Benki ya Posta nchini tangu mwaka 1961 hadi leo kutoka kwa wafanyakazi wa benki hiyo . Wafunzi hao walipata maelezo hayo jana jijini Dar es salaam wakati wa ziara ya mafunzo ya siku mmoja kwenye maonyesho ya 35 ya kimataifa ya biashara ya Dar es salaam. Picha na Tiganya Vincent, MAELEZO_DAR ESALAAM


From http://www.tanzania.go.tz/ministriesf.html...PSPF
ReplyDelete"pspf-tz.org expired on 06/25/2011 and is pending renewal or deletion"
Kaazi kwelikweli!