Waziri wa Kazi na Ajira Mh. Gaudencia Kabaka akisikiliza kwa makini maelezo ya mradi wa ujenzi wa nyumba za bei nafuu kutoka kwa Mkurugenzi wa Uendeshaji Patrick Mongella jana jijini Dar es salaam. Nyumba hizo zinajegwa na Mfuko wa Pensheni kwa watumishi wa umma (PSPF). Waziri huyo na Naibu Wake Dkt Makongoro Mahanga walipata maelezo ya mradi huo wakati walipotembelea banda la Wizara ya Fedha katika maonyesho ya 35 ya kimataifa ya Dar es salaam.
 Juu na chini ni baadhi ya wanafunzi wa kidato cha tano na sita kutoka Shule ya Sekondari ya Morogoro walipata maelezo mafupi kuhusu historia ya Benki ya Posta nchini tangu mwaka 1961 hadi leo kutoka kwa wafanyakazi wa benki hiyo . Wafunzi hao walipata maelezo hayo jana jijini Dar es salaam wakati wa ziara ya mafunzo ya siku mmoja kwenye maonyesho ya 35 ya kimataifa ya biashara ya Dar es salaam. Picha na Tiganya Vincent, MAELEZO_DAR ESALAAM

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 08, 2011

    From http://www.tanzania.go.tz/ministriesf.html...PSPF

    "pspf-tz.org expired on 06/25/2011 and is pending renewal or deletion"

    Kaazi kwelikweli!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...