Kaimu Katibu Mkuu wa TFF,Sunday Kayuni akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam wakati wa kufanya droo ya kupanga tariba ya mashindano ya soka ya vijana chini ya umri wa miaka 17 yafahamikayo kama AIRTEL RISING STARS ambayo yanataraji kuanza rasmi kesho katika viwanja mbali mbali vya jijini Dar es Salaam.Mashindano hayo yatashirikisha timu za kutoka mikoa ya kimichezo ya Kinondoni,Ilala na Temeke huku timu zingine zikitokea mikoa ya Morogoro,Mwanza na Iringa.Kushoto ni Kocha wa Timu ya Taifa (Taifa Stars),Jan Poulsen.
 Meneja Mahusiano wa Kampuni ya simu ya Airtel Tanzania,Jackson Mmbando (katikati) akisisitiza jambo kwenye mkutano huo na waandishi wa habari uliofanyika leo kwenye ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) kabla ya kupangwa kwa droo ya mashindano ya AIRTEL RISING STARS yaliyozinduwa majuma kadhaa yaliyopita na mchezaji wa zamani wa timu ya Manchester United ya nchini Uingereza,Andy Cole alikuja hapa nchini.Kulia ni Meneja Masoko wa Airtel Tanzania,Rahma Mwapachu na kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu wa TFF,Sunday Kayuni.

kwa kuona picha zaidi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...