Abiria wa basi la ng'itu linalofanya safari zake kati ya Mtwara mjini kwenda Dar es salaam,wakiwa wameshuka ndani ya gari hilo kufuatia kuharibika kwa gari hilo katika kijiji cha Mavuji wilayani kilwa hivi karibuni.
Abiria wakiwa wamekata tamaa na wasijue la kufanya baada ya gari walilokuwa wakisafiria kutoka Songea kwenda Masasi mkoa wa Mtwara kuharibika wilayani Namtumbio ambapo walilazimika kusubiri kwa zaidi ya saa 8 njiani kabla ya kuendelea na safari yao.
Abiria waliokuwa wakisafiri kutoka Songea kwenda Masasi mkoani Mtwara,wakiwa hawajui la kufanya kufuatia gari walilokuwa wakisafiria la kampuni ya Kisiwa Video coach,kuharibikia katika kijiji cha Mchomolo wilaya ya Namtumbo mkoa wa Ruvuma,ambapo walilazimika kusubiri kwa zaidi ya masaa 8 bilia ya kupatiwa gari lingine.
Licha ya serikali kugawa vyandarua kwa wananchi kwa ajili ya kupambana na ugonjwa wa malaria lakini baadhi ya wananchi wamekuwa wakitumia vyandarua hivyo kinyume na matumizi kama inavyoonekana moja kati ya chandarua kikitumika kama pazia katika moja ya choo katika kijiji cha Mtandi Kilwa.
Barabara kuu ya Mingoyo - Kibiti ambayo imetumia mamilioni ya shilingi katika ujenzi wake ikiwa imeanza kuharibika ndani ya miaka 2 tangu kujengewa kwake kufuatia mkandarsi aliyejenga barabara hiyo kujenga chini ya kiwango kama inavyooneka ikiwa imeanza kumeguka kingo zake katika kijiji cha kiranjeranje Wilayani Kilwa mkoa wa Lindi.Picha na Muhidin Amri,Globu ya Jamii-Ruvuma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 15, 2011

    wahandishi wa habari muwe na vitu vya maana vya kuandika ni kwli kabisa umeshindwa kuona kuwa net iyo imeshonwa shonwa mala ngapi adi kufikia atua ya kuwekwa apo kma pazia unaamini kabisa kuwa net iyo ingekuwa mzima ingetundikwa apo kwli!kwanza ata vibaka wangeshindwa kuipitia kwli acha siasa kwnye uhandishi wa habari fanya kazi ipasavyo

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 15, 2011

    Sasa chandarua kimeshachakaa unataka mtu aendelee kutumia?

    ReplyDelete
  3. Very good mukhtasari.............tuletee basi za mikoa/wilaya zingine -lol

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 15, 2011

    WAtanzania wenzangu tuelewane kitu kimoja, kwani naona imekuwa ni kuwalaumu wakandarasi kila barabara inapoanza kumeguka! Barabara inapotengenezwa na inapokamilika inahitaji uangalizi na repair kila mwaka, Kwani barabara hiyo ujue kwamba kila sekunde magari ya uzito mbalimbali yanapita usitegemee kwamba barabara hiyo itadumu milele. Ndo maana katika nchi zilizoendelea kila mji unakagua barabara zake na pale kunapokuwa na pot hole wanaziba right away, hawasubiri mpaka barabara igawanyike. Tatizo la Tanzania ni kwamba mkandarasi anapokabidhi barabara kwa serikali basi ndo imetoka serikali haina habari tena ya kuangalia hiyo barabara. Hapo ndo pesa ya walipa kodi inatakiwa kutumika kwa wakandarasi wadogo katika mji.Kwa mtindo huu barabara zitadumu kwa muda mrefu. Ninaamini kabisa hizo barabara zimejengwa katika viwango vya juu kulingana na pesa iliyolipwa. Roads needs daily maintanance. Na barabara ndefu zinahitaji watumiaji kulipa Toll Road Fees japo zinaishia mifukoni mwa watu inabidi serikali kuthibiti hiyo tabia.
    Ndimi mdau

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 15, 2011

    HEEEE DAKIKA TANO KUCHIMBA DAWA

    ReplyDelete
  6. Just curious. Mda uliyeandika insha hapo juu , hii barabara ina miaka mingapia toka imejengwa?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...