Mtanzania mbunifu wa Kizazi Kipya wa mitindo ya nguo Anna Lukindo ametikisa ulimwengu wa fashion jijini london wikiendi iliopita. Anna alionyesha mavazi aliyobuni kwenye maonyesho ya La Geneve North Event, yaliyofanyika
London siku ya ijumaa tarehe 8.7.11.
Ubunifu wa Ann ulipokelewa kwa vifijo na nderemo kwani ulikuwa ndio uliotia fora.
Kulikuwa na wabunifu wengine kumi lakini Anna ndio alikuwa mwafrika na Mtanzania pekee ambaye Mavazi yake yalikubalika na kupendwa na watu wengi zaidi.
Mojawapo ya wageni na wadau mbalimbali walijjitokeza kumpa sapoti Anna ni Mh Balozi wetu Peter Kallaghe na Mama Balozi, Naibu Balozi Chabaka Kilumanga pamoja na watanzania wengine.
Kwa niaba ya URBAN PULSE na GLOBU YA JAMII tunapenda kumpongeza Dada yetu Anna na Kumtakia kila la kheri pamoja na Mafaniko Mema katika fani hii.
Kwa mawasiliano zaidi na Anna tembelea
Anna Luks
Pr/Media:Pauladpope@yahoo.co.uk
Web:www.annaluks.com
Baadhi ya Watanzania waliotokea kumsupport Anna
Model Tina, Anna, Tammy, Zulfa na Rafiki wa Anna
Mamodo wa Anna wakijiandaa kupanda katika kitembea paka.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...