Za leo?
Wanasema waTanzania kazi yetu ni kulalamika weee bila kufanya kitu chochote kubadilisha hali inayotufanya tulalamike. Hatuna haja ya kuwa kama wenzetu wa Misri au Libya, ila leo nimeamua kuwa mTZ tofauti kidogo:mwenye kuanzisha majadiliano ili kinacho nilalamisha kipatiwe utatuzi.  Ninaamini mkiishasoma mtagundua siko pekee yangu mwenye uchungu na huzuni na hasira kuhusu hali ya Muhimbili na utu wa wagonjwa.

Mfano wangu ni wa wadi ya Sewahaji (18), samahani sijui majina vizuri ya wadi za Muhimbili.  Nina uhakika kabisa kwamba Sewahaji hali ni mbaya sana.  Hamna utu wala heshima. Niliona wadi imejaa tokea ubarazani kabla hata ya kuingia wadini.  Kuna wagonjwa sakafuni pande zote mbili.  Wagonjwa wenye hali mbaya: wengine wana damu za masiku na mengineyo ya kibinadamu (sina haja ya kuyataja hapa, nadhani mnaelewa ninachozungumzia).

MaDr hawapiti ipasavyo.  Pengine hiyo hali ya wadini inawavunja moyo japo walikula kiapo cha kuwasaidia wagonjwa iwe itakavyokuwa.  Si kama ninawatetea, wao ndio wangekuwa wa kwanza kuleta mabadiliko, kuleta vurugu ili hali ya wadi na wagonjwa iboreshwe.  Kufikisha malalamiko wizarani.  Waziri wa afya ana hii habari?  Hata yupo?

MaNurse na wenyewe kwa ukosefu wa vifaa vya kufanyia kazi yao, hawafanyi kitu, hata wito hawana.

Mikojo na mengineyo vipo sakafuni kati ya wagonjwa.  MaNurse watapita kukusanya kusanya na kusafisha kijuu juu dakika 30 kabla ya muda wa kuwatembelea wagonjwa hujafika.  Muda mwingine wote sakafu ni chafu na mambo yote hayo.  MaNurse hawana nafasi ya kutosha kusema watapiga deki kona hadi kona kwa sababu wadi ipo imefura na wagonjwa hadi sakafuni.  Harufu hewani ni mbaya sana hata sijui wagonjwa wataponaje.
Mgonjwa anakalishwa na uchafu wake kwa muda mrefu sana.  Yaani utu na heshima (dignity) yake yote inadhalilishwa.

Vyandarua hamna.  Ukitaka chandarua, ni cha mission.  Ukitaka wakufungie cha kwako toka nyumbani, ni mission pia.

Wasafishaji na wenyewe wanadharau wagonjwa.  Kusafisha madirisha wanatumia mpira wa maji uliotoboka toboka.  Bomba la maji ni la bafuni hapo wadini.  Wanavuta huo mpira toka bombani hadi nje ubarazani, huku mpira unawapitia wagonjwa waliolala sakafuni na kuwalowesha.  Roho gani hii? Ni utu kweli?
Ninakuomba Michuzi:

1. Nenda ukajionee, tuma mtu au mtu yeyote mwenye kusoma hii post akajionee. 
2. ui-post hili lalamiko langu "pengine" litaweza kuleta majadiliano ya mabadiliko.  Tusione kitu hakifanyi kazi kabisa tukakaa kimya. 
Maendeleo sio magari na manyumba, sehemu za starehe na vivalo vya nguvu.  Maendeleo ni huduma za afya, usafiri...sitaki nianze kuzungumzia maji na umeme - hio itakuwa post nyingine.....:-\
 
Naomba ufuatilie hili lalamiko, kiubinadamu tu.  Kesho atakuwa ndugu yako kalazwa Sewahaji, sio kama ninakuombea iwe hivyo lakini.  Pengine hatulalamiki kwa sababu hatujui,  Mimi ninajua na nimeona, tusiwe wakimya hata kwenye haki zetu.
Ukae salama.
Mdau Elle.
 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. US BLOGGERJuly 12, 2011

    Dr. US Blogger)

    Hapa ningechafua hali ya hewa lakini naona uchungu hata kusoma. Ila sisi kwenye serikali ya CCM tunajaribu sana kupunguza hizi kero za wananchi kwa kuwahamasisha viongozi katika nyanja zote kuwahudumia wananchi bila ubaguzi

    Nitaomba wahusika washugulikiwe ipasavyo, hii inatia aibu sana

    Dr. US Blogger
    Alumni, Oxford University
    Economics Department

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 12, 2011

    Inasikitisha sana. Mimi nilikuwa sitaki kusoma hii messege lakini wakati mwingine ni vizuri kujua ukweli, hata kama ukweli unauma.
    Hii ndio hali halisi. watu wako very self-centered. Hii ndio tatizo kubwa. Tuombe Mungu atupe moyo wa huruma na kujali watu wengine.
    Thank you mtoa mada and God bless you for speaking the truth.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 12, 2011

    hivi wewe mtoa mada hii unajua hao watumishi wa muhimbili wanalipwa shilingi ngapi?, unajua vizuri kero za wagonjwa wakati mwingine? sisi watanzania ni wachafu sana kwa taarifa yako, hatuna ustaarabu tukiwa wazima sembuse mtu anaumwa?. Mimi nimeshajifungua pale Muhimbili nakwambia uchafu unaofanywa kwa maksudi na wagonjwa bafuni, vyooni utastaajabu. watu wanatupa pamba, matambala waliyotumia kwenye vyoo hivi vya kisasa tena yamejaa damu unategemea nini, wanatema mate ovyo kwenye korido, pembeni ya vitanda hata katika ngazi, uchafu mtupu. Hao manesi nao ni binadamu na tunapaswa kuwarahisishia kazi yao na si kuifanya kuwa ngumu. Malipo wanayopata ni kiduchu ukilinganisha na uzito na unyeti wa kazi yao ambayo pia inawaweka karibu na maambukizi ya magonjwa lukuki. Posho za wabunge kwa siku ndio mshahara wa hawa wahudumu wa afya kwa mwezi, wakati mahitaji na ugumu wa kazi ni mkubwa kuliko hao wabunge wenu. Jaribu kuchunguza upande wa pili wa shilingi na si kulaumu tu. Tunahitaji kubadilika kwanza sisi wenyewe, kuwa na utu na kuheshimu kazi za wenzetu kwa kuwarahishia kazi zao na si kulalamika wakati uchafu ndio jadi yetu. Mtu anatoa haja kubwa chooni na wala hajali kumwaga maji unategemea nini eti nesi aje asafishe uchafu wake. Tubadilike na tuache kuwashutumu hawa watu muhimu kwa maisha yetu.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 12, 2011

    tafadhilini viongozi wetu ogopeni mungu na pia yaliyombele ya macho yenu msijifanye mmevaa miwani ya mbao au kwa sababu wewe na family yako haitogusa hospital za taifa lako la TANZANIA ambalo linaokutilia ujeuli utakwenda kutibiwa nchi nyingine,jitahidini ili mnao waongoza waone jitihada zenu,mfano leo wewe ukiumwa kiongozi utakubali kupelekwa hospital ya taifa na ulazwe chini kama raia mwenzako anae lala chini hivi sasa?utakubali?kama mzalendo wa TAIFA jitahidi mpiga kura wako asilale chinina raia wako asilale chini, HONGERA MIAKA 50 YA UHURU WA TANGANYIKA kwa kurudi nyuma

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 12, 2011

    Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, chini ya Wizara ya Afya iko katika mchakato wa kuboresha idara zake mbalimbali zikiwemo wodi za wagonjwa zifikie viwango vinavyokubalika kimataifa. Mchakato umeanza kutafuta fedha kwa wafadhili kuona namna gani wanaweza kusaidia eneo hilo. mpango huo unatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miaka mitano ijayo

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 12, 2011

    Very sad indeed.
    But has the writer forgotten what the wise ones say:
    A picture is worth a thousand words
    So we are waiting

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 12, 2011

    Viongozi wetu wanatakiwa kuwa na utaratibu wa kutembelea hospitali zetu na kuyaona hayo pengine wataguswa kusaidia na kurekebisha hali hii na kutujali sisi wananchi wao tunaolala sakafuni huku tukiwa hoi kwa kuumwa.

    ReplyDelete
  8. MdauwaSinzaJuly 12, 2011

    MUHIMBILI ingekua iko poa na ina vifaa vyote vya kuuguza, usafi, madawa, net n.k. kama HELA ZILIZOIBIWA KUTOKA EPA, KAGODA, MEREMETA, RICHMOND, TANESCO, WIZARA ZA AFYA, WIZARA YA UJENZI, MALIASILI, RADA, MASHANGINGI, POSHO, SAFARI ZISIZO NA KICHWA WA MGUU, UJENZI WA NYUMBA YA SPIKA, YA GAVANA WA BOT N.K. N.K.
    ZISINGEIBIWA!

    Kasheshe wabongo hatujifunzi, bado tunawapa kura/kula tu, hatuwashikishi adabu wala kuonyesha tumechoshwa na uzembe na ufujaji wa mali za umma kama hivi.

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 12, 2011

    NEXT TIME utakapozungummzia suala kama hili weka PICHA kwani maelezo kama hayo peke yake hayana NGUVU. nenda na simu yako huko wodini chukua picha au VIDEO ili maelezo yawe mafupi kila mtu ajionee mwenyewe kinachoendelea,hivyo ndivyo wanavyofanya watu waliochoshwa na Jambo lolote. get some EVIDENCE AND USE ENTERNET,kila mtu duniani ataona na serikali itachukua hatua muhimu kuhusu hilo kwani itakuwa aibu kubwa kwa serikali tawala hasa ukizingatia kuna WAHISANI WANAOTOA PESA NYINGI KUSAIDIA MAHOSPITALI SASA WAKIGUNDUA KWAMBA WATU HAWAPEWI MSAADA WA KUTOSHA WATAITAKA SERIKALI ITOE MAELEZO. ITS TIME TO STOP BLA BLA BLA. USE MEDIA, USE YA PHONE. KAMA UNAWEZA HONGA KUTUMIA CHANDARUA THEN HONGA URUHUSIWE KUCHUKUA VIDEO.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 12, 2011

    Huyo anony wa jumanne, najua ndio na sisi tunazidi lakini je mimi kama mgonjwa na kujisikia kwangu vibaya, nahitaji kutapika, kutema mate naangalia pembeni kwangu hakuna sehemu maalumu ama kibakuli cha kufanya haya mambo si ntafanya hapohapo nilipo, kuna wakati unaumwa hata kuinuka unashindwa kwa kweli, na kama uongozi wa muhimbili ungehakikisha kila mgonjwa anakuwa na kibakuli maalumu cha kutapika/kutema mate ambacho kiwe kinaoshwa kila siku, au kama hawawezi basi wagonjwa wote wakutapika waje na vyao wenyewe, hii ingesaidia kwenye mambo ya uchafu na maambukizo. Kutupa mabandage ya damu, kama mapipa ya uchafu ya huko bauni/vyooni yangekuwa empty haya yote yasingetokea, mtu unaenda chooni/bafuni bin zimejaa utatupa wapi hizo pad zako? si unaweka pembeni tuu. Alafu, kama hao manurse wangekuwa wanasafisha vyoo/wodi regularly uchafu ungekuwa minimized. Usiwatetee, mtu unaumwa unamuita nurse akusaidie kukuinua anafanya huku amenuna kana kwamba unamsumbua, wengine wanakwambia unadeka, khaa! hawana huruma kabisa, wako very rude. Wodi ya kina mama ndo kabisaaaa usiseme, wakina mama wanonewa utasema hao manurse wao sio wanawake, tena kama mzani ni msichana mdogo ndo kabisa anakuwa bullied na wamama watuwazima na wajukuu kisa kazaa mapema, wanakataza ndugu yako kuingia kwenye chumba cha uzazi ili usione maozo wanayoyafanya wakati wa kumsaidia mama kujifungua. Katika kila wajawazito 10 watano tuu ndo watazaa salama wengine kama sio both mama na mtoto basi mtoto atakufa wakati wa kujifungua, after all that hard work ya kulea mimba 9 months, Wapuuzi manurse kwa uzembe wao mtoto anakufa wakati wa kujifungua, mbaya zaidi hawakwambii sababu, inauma.

    Sio tuu manurse, madoctor service zao utasema wameenda kusomea loliondo? mimi pacha wangu alikuwa na mapacha, siku moja kabla ya kujifungua nikampeleka muhimbili (Fast track "my shoes") kwani alikuwa na dalili za mtoto kuwa na distress, Doctor pumbavu kweli akamrudisha bila hata kumchunguza eti yupo poa, usiku wake siku hiyohiyo tukamrudisha Crapy Fast track Muhimbili, kujifungua mtoto mmoja amefia tumboni withing the last twelve hours. Sasa je kosa ni la nani.

    Mimi naona the whole system ya afya Tanzania inatakiwa kubadilika, Uongozi wa Tanzania uongeze mahospital ili watu wawe wanatibiwa locally, pia manurse na madoctor tutreat wote kama tunavyopenda kuwa treated.

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 13, 2011

    ACHENI MANENO MANENO NA KULALAMA TU IT'S TIME TO TAKE ACTIONS -

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...