Hi Ankal,

Leo majira ya saa moja na dakika 45 nimepanda daladala pale kituo cha moroko kwenda Kawe, bahati mbaya sikupata siti mpaka kwa mwalimu, lakini tangu napanda kulikuwa na mwanafunzi wa kike ameketi katika siti amefunga hijabu lakini alikuwa anaonekana amesinzia, kufika njia panda ya coca cola konda akawa anakusanya nauli kufika kwa yule mwanafunzi akamuamsha lakini binti alikuwa harespond chochote,konda akajua ni usanii labda hataki kulipa nauli, akamtikisa wapi, ndipo watu tukaanza kumsaidia kumuamsha, lakini kumuangalia mapigo alikuwa kimya,ndipo watu wazima walipomcheki wakagundua ameshakufa.

mimi niliteremka kituo cha maringo nikaacha baadhi ya abiria wanaenda kituo cha polisi kawe, kwahiyo wenye watoto wao wanaosoma kawe au maeneo ya huko kama ni wa kike mwenye umri wa kadirio kama miaka 12 wafuatilie

Imenisikitisha sana maana kabinti kamefia usingizini

Mimi Mdau

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 12, 2011

    Innalilah wajnarajuni, inahuzunisha sana ishallah mwenyezi mungu amlaze pahala pema peponi amin, na mungu awape nguvu wafiwa katika wakati huu mgumu sana kwao,

    na mdau ulotowa hii taarifa umefanya jambo la maana sana kutuarifu, safi sana kijana

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 12, 2011

    innalilahi wainna ilayhi rajiun

    ReplyDelete
  3. Inna Lillahi Wainna Illaihi Raajiun,ametangulia nasi tutafuata kwani kila nafsi itaonja umauti na umauti hauna taarifa.Poleni sana wafiwa.Mwenyezi Mungu ailze roho ya marehemu mahali pema Peponi.Amin

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 12, 2011

    INNALILLAH WAINNA ILAH RRAJUYN

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 12, 2011

    Inalilahi wainailahi rajiun! USISIKITIKE SHUKURU MWENYEZIMUNGU KAMCHUKUWA KWENYE HALI SI MBAYA USINGIZINI.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 12, 2011

    inna lilah wainna ilayhi rajiun. Masikini wazazi wake. Mola awape subira Amin.

    Ama kwa mleta taarifa, hivi hukuwa kisheria unatakiwa wewe na abiria wote mliokuwamo ndani ya dala dala hiyo wakati huyo binti alipgundulikana kuwa amefariki kufika kituoni kama mashahidi/kuandika ripoti ya mlichokiona? au ndio bongo watu hawana muda wa kufanya hayo ukuzingatia kuwa hapo polisi hakuna la mara moja?

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 12, 2011

    inna lilah wa inna ilayhi raajiuuna mwenyezi mungu awape moyo wa subra familia yake......!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 12, 2011

    AAAAAAAAAAAAA

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 12, 2011

    innalillah wainnalillah rrajiun.amean

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 12, 2011

    Mungu aiweke roho yake mahala pema peponi

    masikini kweli imenigusa.

    ReplyDelete
  11. Inalillah waina ilaihi rajiuni,mungu amlaze mahali pema ameen

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...