Mkurugenzi wa Clouds Media Group,Joseph Kusaga akimkalibisha mgeni wake,Mwanamuziki mkongwe kutoka nchini Marekani,Chaka Khan aliyewasili leo mchana kwenye viunga vya ofisi hizo.Mwanamuziki huyo anatarajia kufanya onesho lake Julai 23 ndani ya ukumbi wa Ubungo Plaza,kwa udhamini mkubwa wa Club E.
Joe' akimuongoza mgeni wake,Chaka Khan kwenye ofisi yake leo mchana mara alipowasili ndani ya ofisi za Clouds Media Group,zilizopo Mikocheni jijini Dar.
Mwanamuziki Chaka Khan akiwa amepozi kwa picha leo mchana na Mkurugenzi wa kampuni ya Clouds Media Group,Joseph Kusaga akiwa na Mkewe,Mkurugenzi wa kampuni bingwa ya burudani hapa nchini,Prime Time Promotions Ltd Juhayna Ajmi Kusaga pamoja na mtoto wao Natalia Kusaga .
Mkurugenzi wa Clouds Media Group,Joseph Kusaga akimuonesha Mwanamuziki Chaka Khan baadhi ya picha za wanamuziki mbalimbali wa Kimarekani na kwingineko waliowahi kufika nchini Tanzania na pia kufanya kazi na kampuni ya Prime Time Promotions Ltd.
Mwanamuziki Chaka Khan akiacha Chata lake kama ukumbusho wa pekee kwa Kampuni ya Clouds Media Group,huku baadhi ya Wafanyakazi wa kampuni hiyo wakishuhudia tukio hilo adhimu.
"hhhheeeeee yeeeeesssss...!" Mwanamuziki Chaka Khan akigonga na Mtangazaji wa Choice FM,Thandi leo mchana alipokuwa akifanya nae mahojiano mafupi kuhusiana na onyesho lake litakalofanyika ndani ya Ubungo Plaza,July 23 kwa udhamini mkubwa wa Club E.
Mwanamuziki Chaka Khan ambaye ni mtunzi na Muimbaji,aliyeanza kupata umaarufu mkubwa mnamo miaka ya 70,nchini Marekani,akiwa amepozi ndani ya studio za Choice FM mchana huu tayari kwa kufanya mahojiano mafupi kuhusiana na onyesho lake analotarajia kulifanya jumamosi ndani ya Ubungo Plaza,jijini Dar.
Mkurugenzi wa Clouds Media Group Joseph Kusaga akimuonesha Mwanamuziki Chaka Khan baadhi ya picha mbalimbali za wanamuziki waliohi kufika nchini Tanzania na pia kufanya kazi na kampuni hiyo kwa namna moja ama nyingine.
Duh, yaani nampenda sana huyu mama. Natamani ningekuwa bongo nimwone live!
ReplyDeleteJamani, endeleeni ku-enjoy.
HUO NI MFANO TOSHA NA SOMO KWA HAO WANAOJITA MASTAA WA BONGO,MIMI NICHEZA NYIMBO ZA HUYU MAMA TOKA NIKO SHULE YA MSINGI SASA NINA MIKA 50,ENZI ZA DJ MAC-TWIST,EDDY SALLY,CHOGE SLY,KALIKALI,JERRY KOTTO,STAA NA HESHIMA KUJITUNZA NA KUWA NA MAADILI NDIO MANA MPAKA LEO HUYO MAMA MUNEKANO WAKE BADO UNA MVUTO SI MASTAA WETU WANAOJITIA WAZIMU,KUKAA UCHI ULEVI YANI MPAKA WANAKIFU WAMEKUWA KAMA MAZUNGU YA WIKI,HONGERA KUSAGA WEWE NI DJ WA KWELI UMEITOA MBALI CLOUDS TOKA ENZI ZA YMCA MPAKA HAPO MLIPO FIKIA MNASTAILI PONGEZI.
ReplyDeleteKazi nzuri bwana Kusaga ka kuleta hao ma legend
ReplyDeleteOH CHAKA KHAN, THE ONE AND ONLY CHAKA KHAN. WELCOME TO TANZANIA. YOU LOOK MARVELOUS MY DEAR. DON'T FORGET TO VISIT THE GREAT SERENGETI NATIONAL PARK.
ReplyDelete