Timu ya Taifa ya Shelisheli inatarajia kuwasili Arusha kesho mchana (Julai 22 mwaka huu) ikitokea Nairobi kwa ajili ya mechi mbili za kirafiki dhidi ya timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 23.
Mechi hizo zitachezwa Julai 27 na 30 mwaka huu kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid Kaluta, jijini Arusha. Mechi zote zitaanza saa 10 jioni. U23 ambayo iko kambini Dar es Salaam chini ya kocha wake Jamhuri Kihwelo itaondoka Jumapili kwenda Arusha kujiandaa kwa mechi hizo.
Shelisheli inakuja na msafara wa watu 30 wakiwemo wachezaji 24. Wachezaji ni Nelson Sopha, Vincent Euphrasie, Jonathan Bibi, Nigel Freminot, Allen Larue,Ronny Marengo, Gervais Waye Hive, Achille Henriette na Karl Hall.
Wengine ni Alex Nibourette, Jude Nancy, Jones Joubert, Alpha Balde, Nelson Laurence, Trevor Poiret, Henny Dufrene, Don Anacoura, Kevin Betsy, Brian Dorby,Wilnes Brutus, Eugene Valentin, Rashim Padayachy, denis Barbe na Damien Maria.
U23 itaondoka Julai 25 mwaka huu kwenda Arusha ikiwa na kikosi cha wachezaji 20.Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen amewaongeza kwenye U23 wachezaji Juma Seif Kijiko wa Yanga, Haruna Moshi wa Simba na Gaudence Mwaikimba ambaye msimu huu ameombwa usajili Moro United.
Lengo la Poulsen ni kuangalia kiwango cha wachezaji hao ili kuona kama anaweza kuwajumuisha kwenye kikosi cha Taifa Stars ambacho Agosti 10 mwaka huu kitacheza na Palestina katika mechi ya kirafiki itakayofanyika jijini Ramallah. Poulsen atataja kikosi hicho Julai 31 mwaka huu jijini Arusha baada ya mechi hizo mbili.
Pia Kihwelo ametaja kikosi cha wachezaji watakaokwenda Arusha. Wachezaji hao ni Shabani Kado (Yanga), Seif Abdul (African Lyon), Juma Seif (Mtibwa Sugar), Babu Ally (Morani), Shomari Kapombe (Polisi Morogoro), Issa Rashid (Mtibwa Sugar),Salum Kanoni (Simba), Godfrey Wambura (Simba), Jabir Aziz (Azam) na Juma Seif Kijiko (Yanga).
Wengine ni Awadh Juma (Mtibwa Sugar), Haruna Moshi (Simba), Mohamed Soud (Toto Africans), Salum Machaku (Simba), Salum Mnyate (Azam), Khamis Mcha (Azam),Thomas Ulimwengu, Gaudence Mwaikimba (Moro United, Sino Augustino (African Lyon) na Hussein Javu (Mtibwa Sugar).
Mimi kwa maoni yangu,sidhani kama Jamuhuri anajenga timu ya U23,sababu kuna vijana wengi wengi sana mitaani na mikoni ambao wanaweza kuunda timu ya U23 kuliko hivi anavyofanya Jamuhuri kung'ang'ania kuwaita wachezaji wa ligi kuu. Mfano mwaikimba mimi namjua na nimesoma naye yupo kwenye mpira wa ligi kuu tangu mwaka 2000. Chukua mfano mwaka 2000 alikuwa na umri wa miaka 15 mpaka sasa atakuwa na umri wa miaka 25/26,sasa nashangaa jamuhuri anang'ang'ania wazee ambao wapo U40 ila yeye anasema wapo U23.Shabani Kado,Kijiko,Mcha,Mwaikimba etc hawa ni U40 na si U23.
ReplyDelete