Juu na Chini: Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikagua gwaride la heshima lililoandaliwa na jeshi la Ulinzi la Afrika ya Kusini wakati wa mwanzo wa Ziara yake Rasmi ya kitaifa nchini Afrika ya Kusini jana.

Mawaziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Afrika ya Kusini na Tanzania Bernard Membe na Bi. Maite Nkoana Mashabane wakibalishana mikataba ya kuanzishwa kwa Tume ya Ushirikiano(Bi-National Commission) kati ya nchi hizo mbili muda mfupi baada ya kusaini katika ikulu ya Afrika ya Kusini jijini Pretoria jana huku marais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete na Jackob Zuma wakishuhudia.
Rais Dr.Jakaya Mrisho Kikwete akisisitiza jambo wakati yeye na Mwenyeji wake Rais Jackob Zuma walipokuwa wakizungumza katika mkutano na waandishi wa habari katika ikulu ya Afrika ya Kusini jijini Pretoria jana.Rais Dr.Jakaya Kikwete yupo nchini Afrika ya Kusini kwa ziara Rasmi ya Kitaifa ya siku mbili. Picha na Freddy Maro. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 20, 2011

    Serikali yatahadharishwa kuhusu masuala ya ardhi, uraia
    Na Dege Masoli

    Serikali imeshauriwa kuzingatia maoni ya wadau waliyoyatoa wakati wa mchakato wa kutafuta jinsi ya matumizi ya ardhi katika ushirikiano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) katika suala la kutoa ardhi na uraia kwa wananchi wa Rwanda .

    Aidha serikali imetakiwa kuepuka kutoa maamuzi kwa wepesi katika masuala mazito, hasa yanayohusu kulinda maslahi ya wananchi na taifa kwa ujumla.

    Hayo yalielezwa na mwanaharakati wa masuala ya haki za binadamu mkoa wa Tanga, Asseli Shewally, wakati akisisitiza umuhimu wa serikali kufuata maoni ya wadau waliyoyatoa kupinga matumizi ya pamoja ya ardhi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.

    Shewally, alisema kuridhia kutoa ardhi na uraia kwa wananchi wa Rwanda inaonyesha kwamba serikali haikuelewa maana ya wananchi kupinga matumizi ya pamoja ya ardhi ndani ya ushirikiano wa nchi EAC.

    “Suala hili la ardhi na kutoa uraia si la kunong’onezana ni la kitaifa na kulifanya siri ni makosa. Serikali inaonekana kufanya maamuzi kuwa wepesi katika masuala mazito kama haya, jambo ambalo ni hatari kwa mustakabali wa nchi yetu,” alisema Shewally.

    Alisema lengo la wadau kupinga matumizi ya ardhi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki ni kuilinda isichukuliwe na mtu na badala yake itumike kwa manufaa ya wote na vizazi vijavyo na kwamba kuwakabidhi raia wa Rwanda ni sawa na serikali kutoa ardhi kwa mlango wa nyuma.

    Alitahadharisha kwamba, endapo serikali haitakuwa makini na suala la ardhi na ikaendelea kuitoa kama zawadi kwa nchi marafiki athari zake zinaweza kujitokeza miaka 35 ijayo, ambapo maamuzi hayo yataweza kusababisha kuzuka migogoro mikubwa ya kugombea ardhi baina ya wazawa na raia wa kigeni.

    Hata hivyo alimtaka Rais Jakaya Kikwete na serikali kwa ujumla kutambua kwamba nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki zinaimezea mate Tanzania kutokana na fursa mbalimbali zilizopo ikiwemo ardhi na kuwasisitiza Wabunge kuwa wawakilishi wazuri wa wananchi katika kupinga suala hilo.

    CHANZO: NIPASHE

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 20, 2011

    muheshimiwa RAIS wetu KIKWETE tunaomba ushuhulike tatizo la umeme nchini kwetu na liwe historia PLEASEEEEEEE

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...