KUOKOTWA KWA MABOMU YA KIVITA NA KULIPULIWA.
 
Picha na Habari na Pardon Mbwate, wa Jeshi la Polisi- Kigoma

 
Jeshi la Polisi mkoa wa Kigoma kwa kushirikiana na Maafisa wa JWTZ jana walifanikiwa kulipua mabomu manane  na yaliyogundulika kufichwa kwenye kichaka kimoja karibu na Kambi ya wakimbizi wa Burundi ya Mtabila wilayani Kasulu mkoani humo.
 
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma ACP Fraisser Kashai, amesema kuwa mabomu saba kati ya hayo yamegunduliwa na watoto waliokuwa wakichuma matunda katika eneo hilo na baadaye kutoa taarifa kwa uongozi wa eneo hilo na kuwajulisha Polisi wa operesheni na lingine liligundulika katika eneo la bandari ya Kigoma mjini.
  
Kamanda Kashai amesema kuwa baada ya Polisi kupata taarifa za kuwepo kwa mabomu hayo ambayo yalikuwa yamefichwa kichakani, walifika katika eneo hilo na kubaini kuwa mabomu hayo yalikua hayajalipuka.
 
Aidha Kamanda amesema kuwa Polisi walipofika katika eneo hilo pia waligundua risari 48 zinazotoa mwanga ambazo zinatumiwa na askari walipo katika mapigano kwenye uwanja wa vita.
 
Amesema baada ya kubaini hayo yote, Askari hao waliwasiliana na Uongozi wa Polisi Mkoa Kigoma ambapo nao walichukua hatua ya kuwajulisha wenzetu wa Jeshi la Wananchi na kupatiwa wataalamu wa milipuko na kuongozana na Polisi hadi katika eneo la tukio.
 
Amesema walipofika Maafisa hao walifanya uchunguzi wa kujua aina na uwezo wa mabomu hayo na baadaye kuyalipua kitaalamu na kuepusha madhara.
 
Kamanda huyo amesema kuwa Vyombo vya Ulinzi na Usalama mkoani humo, vinaamini kuwa kama mabomu hayo yangelipuka yangeweza kuleta hatari kubwa ikiwa ni pamoja na kuhatarisha maisha ya wakazi wa eneo hilo wakiwemo watoto.
 
Kwani amesemakuwa kama mabomu hayo yangechezewa ama kukanyagwa kwa bahati mbaya yangeweza kulipuka na kuleta madhara makubwa kwa wananchi.
 
Amesema Vyombo vya Ulinzi na Usalama vinaendelea kufanya uchunguzi kujua waliohusika na uwekaji wa mabomo pamoja na sisari hizo ili kuwachukulia hatua za kisheria.
 
Hata hivyo Kamanda Kashai amesema kuwa Vyombo vya Ulinnzi na Usalama mkoani humo kwa pamoja, vimewapongeza wananchi waliotoa taarifa hiyo na kuwaomba wengine kuioga mfano huo kama hatua ya kunusuru maisha ya wananchi wetu kuepuka madhara ya milipuko.
 
Amewahakikishia wananchi wa eneo hilo na mkoa mzima wakiwemo wakimbiizi kuwa eneo lililogundulika mabomu hayo hivi sasa ni salama na waendelee na shughuli zao kama kawaida na kutosita kutoa taarifa pale wanapobaini kitu wanachokitilia mashaka ili kichukuliwe hatua,.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...