Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhandisi Pius Msekela (Wa pili Kulia) akiangalia ubora wa simu 20, Tshirt 300 na fedha taslimu shilingi milioni 15/- alizopokea kutoka kwa Meneja Mauzo wa Vodacom Tanzania kanda ya kati Macfaydyne Minja zitakazotumika kwa ajili ya mawasiliano na maandalizi ya Maonesho ya Nanenane mwaka huu. Anayeshuhudia (Katikati) ni Atilia Lupala ambaye ni Mkuu wa kanda ya Pwani wa kampuni hiyo na kulia ni Dk Samson Muniko Katibu wa Taso kanda ya kati . 
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhandisi Pius Msekela ( Kulia) akimsikiliza Mtaalam wa Masuala ya Habari wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu (Wa pili kushoto) wakati wa hafla ya makabidhiano wa simu 20, Tshirt 300 na fedha taslimu shilingi milioni 15/- zitakazotumika kwa ajili ya mawasiliano na maandalizi ya Maonesho ya Nanenane mwaka huu. Wengine ni Meneja Mauzo wa kampuni hiyo kanda ya kati Macfaydyne Minja (Kushoto) na Atilia Lupala ambaye ni Mkuu wa kanda ya Pwani 

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhandisi Pius Msekela ( Kulia) akiteta jambo na Wafanyakazi wa Vodacom Tanzania (Kutoka kushoto) na Meneja Mauzo kanda ya kati Macfaydyne Minja, Atilia Lupala ambaye ni Mkuu wa kanda ya Pwani na Mtaalam wa Masuala ya Habari wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu wakati wa hafla ya makabidhiano ya simu 20, Tshirt 300 na fedha taslimu shilingi milioni 15/- zitakazotumika kwa ajili ya mawasiliano na maandalizi ya Maonesho ya Nanenane mwaka huu. (Picha kwa Hisani ya Vodacom.)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 23, 2011

    Macfaydyne uko juu my brother.......go vodacom

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...