Wazalendo,
Naomba kuchukua fursa hii kuwashukuru wote waliojitokeza kwa hali na mali kushiriki katika msiba huu.
Pia naomba niwataarifu kuwa michango yetu ya rambi rambi hadi sasa ni Tshs. 585,000/= na tunatarajia kuipeleka kwa familia ya marehemu siku ya Jumapili tarehe 24/07/2011 saa 5 asubuhi.
Hivyo basi naomba nitoe wito kwa wote watakaopenda kuchangia wafanye hivyo kabla ya siku hiyo yaani mwisho wa kupokea rambi rambi ni jumamosi saa za kazi na baada ya hapo tutaziweka bank kwenye account ya mjane na wale watakaopenda kuwepo siku hiyo ya jumapili tutakayokwenda kumkabiddi mjane deposit slip basi tukutane pale BP Mwenge Petrol Station saa 4.00 asubuhi ili twende kwa pamoja.
Siku hiyo tutkuwepo sisi TPN na kutakuwa pia na kundi jingine la marafiki wa marehemu linaliongozwa na Mike Mjinja ambao nao wanachanga na tutaungana nao kukabidhi rambirambi hizi.
Nawashukuru wote naomba tuendelee kushirikiana kwa hali na mali wakati wa raha na shida.
Mungu awabariki.
Phares Magesa
Raisi- TPN

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...