Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI Mh. Kassim Majaliwa |
NA MAGRETH KINABO – MAELEZO,DODOMA
SERIKALI imepeleka kiasi cha fedha cha sh. bilioni 15.5 katika halimashauri zote nchini kwa ajili ya likizo na uhamisho kwa walimu wa shule za msingi na sekondari katika kipindi cha mwaka wa fedha wa 2010/2011.
Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,TAMISEMI) Kassim Majaliwa wakati akijibu swali na mbunge wa Jimbo la Singida Mjini, Mohamed Dewji(CCM) .
Ambalo lililoulizwa na mbunge wa Viti Maalum(CCM) Singida , Diana Chilolo kwa niaba yake ambaye alitaka kufahamu kuwa serikali ina mapango gani wa kumaliza malalamiko yanayohusu stahili za walimu wa shule za Singida na kungineko nchini.
Akijibu swali hilo Naibu Waziri huyo alisema kati ya fedha hizo sh.milioni 475.3 zilipelekwa katika mkoa wa huo, ambapo sh.milioni 388.8 ni kwa ajili ya likizo na sh.milioni 68.5 kwa ajili ya uhamisho.
Aliongeza kuwa serikali kwa wakati tofauti imekuwa ikichukua hatua mahsusi ili kuhakikisha kwamba inamaliza malalamiko hayo ya stahili mbalimbali, ambapo mwaka 2009 ili hakiki na kulipa madeni ya walimu , jumla yash. bilioni 32.2 zilitolewa kulipa stahili za walimu wa shule za msingi na sh. bilioni 12.5 kwa stahili mbalimbali za walimu wa shule za sekondari nchini.
Waziri Majaliwa alisema kuanzia mwaka 2009/2010 ,serikali imeweka utaratibu ambao walimu wanapangwa wanalipwa mishahara na stahili zao mara wanaporipoti katika mamlaka ya Serikali za Mitaa. Hivyo ili kufanikisha azma hiyo Februari mwaka huu ilipeleka katika halimashauri zote nchini jumla ya sh. bilioni 15.3 kwa ajili ya malipo ya posho ya kujikimu, nauli, mizigo na wategemezi kwa walimu wapya.
Aidha alisema serikali imetoa maelekezo kwa wakurugenzi wa halimashauri zote nchini kutozalisha madeni na kuzingatia maelekezo ya serikali kwa kulipa stahili za likizo, uhamisho na matibabu.
Alisema madeni ya walimu wa mkoa huo na nchini kote stahili zao zinashughulikiwa na zitalipwa baada ya taratibu kukamilika.mwisho.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...