BALOZI WA TANZANIA NCHINI URUSI MH. JAKA MWAMBI AKIZUNGUMZA NA WANAFUNZI WALIOMALIZA MASOMO YAO NCHINI URUSI

UBALOZI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ULIOPO MOSCOW NCHINI URUSI UMEFANYA HAFLA FUPI YA KUWAAGA WANAFUNZI WALIOHITIMU MASOMO YAO NCHINI URUSI. KATIKA HOTUBA YAKE KWA WAHITIMU HAO, BALOZI WA TANZANIA NCHINI URUSI MH. JAKA MWAMBI AMEWAASA WAHITIU HAO KUZINGATIA TAALUMA WALIOIPATA KATIKA KUENDELEZA TAIFA LA TANZANIA.

MH. MWAMBI AMESEMA SASA KUNA USHINDANI MKUBWA KWENYE SOKO LA AJIRA KUTOKANA NA UMOJA WA AFRIKA MASHARIKI. AMEWATAKA WAHITIMU HAO KUWA NGANGARI NA KUVUMILIA BAADA YA KURUDI NYUMBANI KWANI MWANZO NI MGUMU.

KATIKA HOTUBA YAKE ILIYODUMU KWA MUDA WA DK. 48, MH. BALOZI ALISISITIZA KUTOPOTEZA MUDA MWINGI KATIKA KUCHAGUA KAZI BALI KURIDHIKA NA KILE AMBACHO KITAPATIKANA MARA TUU WATAKAPORUDI NYUMBANI TANZANIA.

KATI YA WANAFUNZI WALIOHITIMU MASOMO YAO WAPO WALIOSOMEA TOURISM, HOSPITALITY AND SERVICE, MEDICINE, PHARMACY, ENGINEER NA ECONOMICS.
SEHEMU YA MAAKULI MARA BAADA YA HOTUBA YA MH. BALOZI

BAADA YA HAFLA HIYO FUPI ILIYOANZA MAJIRA YA SAA SABA MCHANA NA KUMALIZIKA SAA KUMI NA MOJA JIONI ILIKUWA NI HEPI BETHIDEI YA KUZALIA KWA MJUKUU WA BALOZI WA TANZANIA NCHINI URUSI MH. JAKA MWAMBI.
MTOTO DANIELA ALIYETIMIZA MWAKA MMOJA
MTOTO AKIWA ANATEMBEA
MAMA MZAZI WA MTOTO PROSCOVIA MWAMBI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. NAAAAM NIMEIPENDA HII KWA MHESHIMIWA JAKA MWAMBI KUTAMBUA UMUHIMU WA WASOMI WETU HASA WA WAZAWA WA TAIFA HILI KUWAPA SAPORI HIYOO NAAMINI NA VIONGOZI WENGINE WATAIGA MFANO WAKO .MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU MMBARIKI JAKA MWAMBII AMEEN

    ReplyDelete
  2. TUMEIPENDA SAAAN HASA SISI WAZAWA WA KITANZANIA .TUMEFURAHI KUONA KIONGOZI WETU MHE SHIMIWA JAKA MWAMBI AMETAMBUA UMUHIMU WA SASOMI WETU KWA KUWAPA FARAJA NA MANENO YENYE BUSARA SAAAN
    TUNAAMINI KUA NA VIONGOZI WENGINE PIA WATAIGA MFANOO WAKO HONGERA SAN MH JAKA MWAMBI MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU MMBARIKI JAKA MWAMBI.

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 12, 2011

    Imenifurahisha sana kuona Balozi wa urusi akiwapa support na kuwaalika vijana wa Taifa lake baada ya masomo yao lakini pia inasikitisha sana kwa Balozi wetu nchini India si kuwaalika na kuwapa maneno mazuri wahitimu bali pia hata akialikwa kwenye Graduation za wanafunzi wa Kitanzania huwa hafiki wala hatumi mtu yeyote kumuwakilisha, mbali na hayo kumetokea misiba ya wanafunzi wasiopungua watatu hakuja Balozi wala kutuma mtu hapa Hyderabad hii inasikitisha sana na naomba Uncle usiibanie hii huenda ujumbe ukafika, Balozi wetu wa India hawajibiki ipasavyo ikizingatiwa kuwa Watanzania wengi tunaoishi India ni Wanafunzi...

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...