Habari za saa hizi Mabibi na Mabwana.

Ufuatao ni utabiri wa hali ya Umeme kwa siku ya leo!
Pepo za umeme zitavuma taratibu kutoka upande wa kusini mwa Dar es Salaam kuelekea upande wa Kaskazini, hivyo kutakuwa na umeme mchache maeneo yote ya Jiji na ngurumo nyingi za Jenereta pande za Kivukoni, Kariakoo, Pugu road, Mwenge, Posta na maeneo yote ya katikati ya jiji la Dar es Salaam.

Na kwa wakati wa usiku watu wa Mbagala, Kigamboni, Kimara, Mtoni na maeneo yote ya jirani wilaya ya Temeke na Kinondoni kutakuwa na Kiza kisichojulikana mwisho wake ........ 

Maeneo ya Sinza, Mbezi na Tegeta kutakuwa na miunguromo ya jenereta hapa na pale nyakati za usiku , hii ni kutokana na familia chache zinazotumia jenereta nyakati za usiku.

Ni mtabiri wenu kutoka mamlaka ya utabiri wa nguvu za umeme Ubungo Tanesco ghorofa ya Pili ....... 

Nawatakia siku njema. 
Ahsanteni.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 12, 2011

    Yesuu na Maria!! uwiiiiii...Nilikuwa na hasira leo, lakini baada ya kusoma huu utabiri wa hali umeme nimejikuta naangua kicheko.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 12, 2011

    Du hi kali

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 12, 2011

    hahhahaaaaa soooooo funny!!! Tanzania Bila Umeme Haiwezekani. Natumaini tatizo litapatiwa ufumbuzi karibuni. Mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 12, 2011

    This just made my day.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 12, 2011

    HAHA, VELE VELE CLEATIVE(creative)!....na hiyo ndo hali halisi Hongera kwa utabiri!

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 12, 2011

    uhhuuuu,,huuuuiiiiiiiiiii,bhajameniiii.kumbe tunaweza kuwa na wachekeshaji na watu wa ku-tutoa tension??? ebu ngoja nikae vizuri kwanza!!samahani wewe ni binti au kaka??nina zawadi yako kwa utabili huu wa hali ya umeme.Japo kuwa ulitakiwa ushirikishe na pepo za mbalamwezi zitakazovuma maeneo ya tungi,hivyo kusababisha mwanga mchache maeneo ya tungi shule ya msingi........haha haha...ha...
    Utakapoeleza jinsia yako!!tumia mail thinkers_global@yahoo.com. utapata zawadi bila shida!!

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 12, 2011

    Juzi mitaa ya kati mimi na msela wangu (ndio kwanza kapata kazi, hata wiki 3 bado) tumeingia bar flani Temeke, nikamtambulisha jamaa kwa masela wangu wa huko....jamaa hawakumuunga wala nini, disaini walimkaushia flani, mara baada ya kulewa lewa wakaanza kumuambia atimke fasta na wasimuone tena karibu nao, kisa jamaa anafanya kazi TANESCO. Nilishindwa cha kufanya na kumshauri aondoke tu ili lisijetokea la kutokea. Hali inazidi kuwa mbaya.

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 12, 2011

    nice one,you really made my day

    ReplyDelete
  9. AnonymousJuly 12, 2011

    Wadau huu utabiri wa hali ya umeme ni "Bab Kubwa!!!"
    Nimejikuta naangua kicheko pekeyangu huku ugenini.

    ReplyDelete
  10. AnonymousJuly 13, 2011

    Hii ya leo kali

    ReplyDelete
  11. AnonymousJuly 16, 2011

    Yaaaani,hakika hii ni babu kubwa kweli kweli,japo imenivunja mifupa kwa kucheka sana lakini ukweli ndo huo na bila shaka ujumbe umefika.Sirikali mpo jameni??????
    Tanzania Tanzania

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...