Mwenyekiti wa Chama cha Wanamuziki Tanzania (Tanzania Flava Unit),Hamis Mwinjuma  a.k.a Mwana FA (katikati) akizungumza na waandishi wa habari juu ya uzinduzi wa video yao mpya inayohusiana na sherehe za miaka 50 ya uhuru wa Tanzania,mkutano huu umefanika mchana huu,Leaders Club,jijini Dar.Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Chama Hicho,Khalid Mohamed (T.I.D),na kushoto ni Mjumbe wa Chama hicho,Khadija Shaaban Keysher.
Msemaji Mkuu wa Tanzania Flava Unit,Said Fella a.k.a Mkubwa Fella akiwatambulisha viongozi waandamini wa chama hicho,mapema leo kwenye viwanja vya Leaders Club,Kinondoni jijini Dar.
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kwenye mkutano huo leo.
Wasanii pamoja na waandishi wa habari wakiiangalia video hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 20, 2011

    Nimeangalia video hii nadhani wasaanii wameshindwa kuwa kioo cha jamii, kwa sababu hiyo miaka 50 wanayoimba sifa zake haiendani na hali halisi ya maendeleo. Wanaimba amani bila kujua Tanzania hakuna amani, japo hatyupo vitani lakini watu tuko kwenye woga na watu wanauwa na vyombo vya dola mfano ni kule mkoani Arusha na Mara mwaka huu, Zanzibar wakati wa uchanguzi, watu tunaishi maisha ya kuvamiwa na majambazi, hakuna maendeleo japo wanaimba tulikuwa gizani sasa tuko kwenye nuru wakati nchi iko kweny kiza cha umeme maendeleo ukishuka, wanasema tumejaliwa mali nyingi lakini ni wangapi wanazifaidi kama siyo kwamba zimeuzwa kwa wageni na wananchi wakibaki kwenye lindi la umaskini, ufisadi umekomaa, wale maadui maradhi ujinga na umasikini ukizidi kukua kila kukicha, juzi tumeambiwa tunaongoza katika Afrika mashariki kwa watoto kumaliza bila kujua kusoma, hospital hakuna dawa magonjwa madogo yanaua watu, tuna mali inaliwa na wachache. Nadhani wanatakiwa waone mbali badala ya njaa ya kuimba ili wasifiwe na watawala

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 20, 2011

    ni video nzuri ila iatpendeza zaidi kwa siku zijazo wakieleza pia na changamoto zinazotukabili kwa sasa pia, kama rushwa, ufisadi na magonjwa

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 20, 2011

    Political....

    Basically, Tanzania haikupata uhuru. Tanzania ilizaliwa 1964 tarehe 26 April. Ni uhuru wa Tanganyika ndio ilikuwa nchi wakati huo na ndio ilipata uhuru.

    Tusipotoshe ukweli. Let us do not politicize the truth. Ni miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika.

    2014 tutasheherekea miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na hapa tutasema miaka 50 ya uhuru wa zenji(ilikuwa 12 Januari 1964) na 50 ya muungano.

    Pia wasanii msikimbilie kutoa sifa ambazo hazipo...

    Shortfalls ni sehemu ya mafanikio. Lets us do comperative analysis ili tujione tuko wapi tukijilinganisha na nchi nyingine za calibre yetu.

    Je elimu yetu ni bora zaidi sasa kuliko wakati wa miaka 50 iliyopita, je huduma za jamii(afya, usafiri wa umma, huduma za ardhi, huduma zinginezo) zimeboreka au zimedidimia? Rushwa je?

    Uchukuzi (reli imekufa, ndege za nchi zimekufa, meli za nchi ziko hohehahe), je tumeenda mbele hapa au tumerudi nyuma???

    Barabara tumejitahidi, lakini kwa miaka hamsini ni hizo kilometers tu ndio tumeweza kuafanya??? Nafikiri ilitakiwa iwe zaidi...

    Umeme na maji, tumeenda mbele au tumerudi nyuma? nafikiri tumerudi nyuma...

    Mawasiliano, shirika la taifa TTCL sasa hivi ni shirika mbadala.... Haikutakiwa kuwa hivi hata kidogo... Tumekosea wapi????

    Vipi kilimo, bado ni uti wa mgongo??? mkulima wa sasa wa hali ya chini(jembe la mkono) ni bora kuliko yule wa miaka ya 60? Hali yake imeenda ikiboreka au ikiharibika zaidi????

    Kule kwenye uvuvi je tumenufaikaje kwa kuwa na bahari kwa miaka hamsini?? Huduma za bandari je ?????

    Turudi pale mwalimu aliposema wayaache watanzania wakisoma watayachimba, je tumenufaika vipi na madini???? Tumeenda mbele au tumerudi nyuma? Je tumeiishi ndoto ya Mwalimu kwa kuwa tumeshasoma? Wasiwasi wangu ni kwamba tumesoma wengi lakini ni wachache sana wameelimika.

    Amani ya kweli inapatika ndani ya mtu, jiulize una amani ya kweli wakati ukienda kuomba hati ya kiwanja ulichonunua kwa inflated price inabidi utoe hongo mpaka uchanganikiwe? Unapotaka huduma yoyote serikali kuu ni lazima utoe chochote tena kisicho cha kitaratibu (namaaniasha hongo)?

    Msanii una amani gani wakati kazi zako zinaibwa kila siku na unalalamika? Mfanyakazi una amani gani wakati wewe ndio mlipakodi halisi huku mfanyabiashara ana mapato zaidi na halipi kodi halisi?

    Pia ewe muajiriwa uliyeko dar es salaam, una amani gani kwa foleni hii iliyopo??? wengi waishio pembezoni mwa jiji, kimara, mbezi zote, bunju, tegeta, airport,segerea, tabata, mbagala etc wanatoka usiku nyumbani na kurudi usiku nyumbani... hao watoto mnawaona saa ngapi? je mna amani kutokuona watoto wenu wakikua ???

    Mtanzania ana amani gani wakati anauziwa vitu fake na substandard kwa bei ya genuine product? Maana si kila mtanzania ana uwezo wa kwenda dubai na china na ulaya kufanya shoping.

    NI MAWAZO TU WADAU... Nilikuwa nafikiri kwa sauti tu ....

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 20, 2011

    SEMENI UHURU WA TANGANYIKA SIO TANZANIA KWA VILE ZANZIBAR HAWAJAFIKISHA MIAKA 50 TOKEA WAPATE UHURU WAO 1963....NA TANGANYIKA WALIPATA UHURU WAO 1961

    MKUU USIIPOTEZE HISTORY YA TANGANYIKA SIO VIZURI KUWADANGANYA VIZAZI VETU BORA TUWEKE UKWELI NA WAO WAFAHAMU!!!

    ReplyDelete
  5. Nauliza uhuru wa Tanzania au TANGANYIKA ? Mbona munatuchanganya hapa ? Tanganyika imepeta uhuru 1961,na muungangano wa tanganyika na zanzibar 1964,sherehe ipi inayosherekewa ?

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 20, 2011

    Nadhani Michuzi hawa wasanii hawaendi na wakati au shule imewapiga chenga. Tunatimiza miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika na siyo Tanzania, rudi mkafanye editing ya wimbo wenu. Pili wapi tumeendelea kama maisha ni shida tupu, hakuna matibabu kwa wagonjwa bado wanakufa na malaria na magonjwa ya kuhara wakati nchi zenye miaka 50 ya uhuru ni hadithi, kiwango cha elimu kimeshuka East Africa, hakuna mawasiliano ya anga ATC imekufa, hakuna reli, barabara mijini ni foleni tupu, na zilizotegenezwa si za kiwango cha miaka hiyo, hakuna amani ya binafsi ya ya jumla, amani gani mtu maisha yanakwenda kombo, amani gani vibaka na majambazi kila mahali, amani gani democrasia ni kwa mtutu wa bunduki, amani gani mtu ana uhakika wa kupeleka mtoto wake shule richa ya kumpa mlo wa kawaida, amani gani mtu anasumbuliwa na umaskini wa kutupwa. Je wanasema tumetoka gizani tuko kwenye nuru, nuru gani Tanesco nchi iko gizani, nuru gani mtu ana uhakika wa maisha ya kesho, nuru gani kila kukicha mafisadi wanatubana mbavu, wezi kutoka nje wanachota mali yetu ya asili kama sisi hatuna akili nzuri.
    Wasanii rudi mkafanye kazi hii upya msituletee uchuro au uchafu wenu hapa

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 20, 2011

    Kusema Tanzania kuna amani dunia nzima its a heavy statement na kuitimizia si kirahisi ukizingatia kuwa sio ukweli kiihivyo!

    ReplyDelete
  8. AnonymousJuly 29, 2011

    JAMANI NUSU YA BENDERA KWENYE HIYO VIDEO ZIKO JUU CHINI, YAANI KUNA SEHEMU KUNA WATU WAWILI KILA MMOJA AMESHIKA BENDERA YENYE MTAZAMO WAKE. ATER 50 YEARS OR IS IT 57 YEARS BADO HATUJUI BENDERA YETU INATAKIWA KUSHIKWAJE. KWA KWELI PRODUCER WA HII VIDEO, WAIMBAJI NA HAO WOOOTE WALIOSHIKA BENDERA KWENYE VIDEO BURE KABISA. HIVI SIO KOSA LA JINAI KUSHIKA BENDERA JUU CHINI, MBONA HII VIDEO INA KASHIFU, KICHEFUCHEFU, WATANZANIA HAOOOOOO ETI PROUD OF TANZANIA HALAFU KASHIKA BENDERA JUU CHINI...............

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...