Na Mwandishi wa Jeshi la Polisi –Zanzibar
Viongozi sita wa madhehebu ya dini wanaojihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya nchini, wamejitokeza mbele ya Kamati ya Maadili ya Viongozi wa Dini na Haki za Jamii na kukiri kujihusisha na biashara hiyo kwa muda mrefu sasa.
Afisa Uhusiano wa Jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta Mohammed Mhina, amesema kuwa baada ya kuhojiwa, Viongozi hao waliiomba Kamati hiyo kutowataja hadharani majina ama madhehebu yao kwa kuhofia kubezwa kwa madhehebu wanayoyaongoza.
Akizungumza mwishoni mwa ziara yao Visiwani humo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mchungaji William Mwamalanga wa Kanisa la Pentekosti Tanzania, amesema kuwa orodha hiyo na nyingine ya watu 18 wakiwemo wafanyabiashara wakubwa na Wanasiasa wanaojihusisha na biashara hiyo haramu zote zitafikishwa kwa Mkuu wa kitengo cha Polisi cha Kupambana na dawa za Kulevya nchi.
Mchungaji Mwamalanga amesema kuwa, tatizo la ongezeko la dawa za kulevya pia inazihusu nchi mbalimbali duniani na kwamba kamati hiyo itakutana na kamati nyingine kama hizo za nchi za Maziwa Makuu kwa maana ya Afrika ya Mashariki kuzungumzia ufumbuzi wa suala hilo.
Amesema mkutano huo pia utapendekeza kwa mabunge ya nchi hizo na Bunge la Afrika ya Mashariki kutunga sheria za kuwafilisi wale wote waliojilimbikizia mali kutokana na biasha za dawa za kulevya kwa nchi wanachama.
Hata hivyo Kamati hiyo ya Maadili ya Viongozi wa Dini na Haki za Jamii ikiwa hapa Visiwani, imesifu na kupongeza juhudi za Jeshi la Polisi kwa hatua zao za kukabiliana na ongezeko la dawa za kulevya.
Akizungumzia kero ya dawa za kulevya visiwani hapa, Kamanda wa Polisi mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar ACP Aziz Juma Mohammed, amesema kuwa Jeshi hilo limekuwa likiwakamata wengi wa wafanyabiashara na watumiaji wa dawa za kulevya na kuwafikisha mahakamani.
Hata hivyo, kamanda Aziz ametoa wito kwa wananchi na wadau mbalimbali wa usalama kuendelea kusaidiana na Jeshi hilo kwa kutoa taarifa za wale wote wanaojihusisha na mtandao wa dawa hizo.
Kamanda Aziz amesema kama kila mwananchi atatoa taarifa za siri Polisi za kuwepo kwa mtu ama kundi la watu wanaojihusisha na biashara hiyo ama uhalifu mwingine wowote, ni wazi kabisa kuwa Polisi iyawatia mbaroni.
Wiki iliyopita watu wawili wakazi wa Jijini Dar es Salaam, wamekamatwa kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar kwa nyakati tofauti wakitokea nchini Brazil ambapo kila mmoja alipatikana na kiasi kikubwa cha madawa ya Kulevya aina ya Cocaine.
Wagala wakiambiwa kwamba mnauza nyunga wanakasirika. Haya angalieni sasa. Tunataka muwataje na madhehebu yao yote. Zanzibar ni nchi ya kiislamu na hawa wote lazima warudi kwao bara.
ReplyDeleteKaka issa, naomba nichukue nafasi ya pekee kuishukuru blog yako kwa habari ambazo kamwe huwezi kuzipata kupitia vyombo vingine, naomba pia nimkosoe mchangiaji aliyechangia hapo awali kwa kuhusisha wauza unga na ukristo huku akiwataja kuwa ni wa kutoka Tanzania bara, si kweli naamini hata waislam tena wengine toka zanzibar wanafanya biashara hii kama si tanzania basi nje ya nchi, naomba vita hii isiishie kwa viongozi wa dini bali mahakamani, mchungaji huyu wa pentekoste asipowataja kwa watanzania, wananchi kupitia mitandao na media nyingine tutahakikisha sheria inachukua mkondo wake na sio porojo zenu zenye mwelekeo wa kisiasa, bila kuwajuwa viongoz wa dini wanaouza unga basi mchungaji umejipalia makaa ya moto, wananchi tutakufa na nyinyi mnaohudhuria huko zanzibar. Ni WAKATI serikali kutenga kiasi fulani kwa mtu atakaesaidia kukamatwa wauza unga na sio porojo tu kwani watu hawa ni matajiri na wanamitandao inayowalinda, ukifuatilia yaliyowahi kujili Jamaica juu ya vita kati ya serikal na wauzaunga utagundua kuwa si vita ndogo inahitaji pesa na akili kwani wengine wako karibu sana na wananchi kiasi kwamba wananchi walikuwa tayari kuiacha serikal yao na kuungana na muuza unga aliyekuwa msaada mkubwa kwa wananchi wake kuliko serikali yao, Pesa ya nchi itumike kuudhibiti mtandao mzima. Nawasilisha kwa IGP MWEMAKaka issa, naomba nichukue nafasi ya pekee kuishukuru blog yako kwa habari ambazo kamwe huwezi kuzipata kupitia vyombo vingine, naomba pia nimkosoe mchangiaji aliyechangia hapo awali kwa kuhusisha wauza unga na ukristo huku akiwataja kuwa ni wa kutoka Tanzania bara, si kweli naamini hata waislam tena wengine toka zanzibar wanafanya biashara hii kama si tanzania basi nje ya nchi, naomba vita hii isiishie kwa viongozi wa dini bali mahakamani, mchungaji huyu wa pentekoste asipowataja kwa watanzania, wananchi kupitia mitandao na media nyingine tutahakikisha sheria inachukua mkondo wake na sio porojo zenu zenye mwelekeo wa kisiasa, bila kuwajuwa viongoz wa dini wanaouza unga basi mchungaji umejipalia makaa ya moto, wananchi tutakufa na nyinyi mnaohudhuria huko zanzibar. Ni WAKATI serikali kutenga kiasi fulani kwa mtu atakaesaidia kukamatwa wauza unga na sio porojo tu kwani watu hawa ni matajiri na wanamitandao inayowalinda, ukifuatilia yaliyowahi kujili Jamaica juu ya vita kati ya serikal na wauzaunga utagundua kuwa si vita ndogo inahitaji pesa na akili kwani wengine wako karibu sana na wananchi kiasi kwamba wananchi walikuwa tayari kuiacha serikal yao na kuungana na muuza unga aliyekuwa msaada mkubwa kwa wananchi wake kuliko serikali yao,
ReplyDeleteMazingaombwe matupu. Sasa kwanini wasitajwe na kufikishwa mahakamani?? Nchi ina sheria, sasa nyie mmewakamata halafu mnasema tumewakamata bila kuwafikisha mahakamani na tena wanawaambia msitutaje majina. Sasa hii nchi inaenda wapi? Mtuhumiwa yaani ana amrisha jinsi sheria itakavyokuwa? Sijawahi kuona sehemu yeyote duniani.
ReplyDeletekutangaza injili kwa nyunga. lazima watumie njia yeyote ili mradi injili iende.
ReplyDeletekubwisha wanetu.
1- Wewe anoy wa kwanza hebu nyamaza kwanza usirukie mambo ambayo unaweza kuja kuona aibu.Tayari umewatia kichwani waliohusika ni dini gani.Sasa je wakijakutajwa kama ni waisilamu utafanyaje?
ReplyDelete2-Kumbe kikwete aliongea ukweli mtupu na watu wakaanza kuchonga eti kwasababu aliyasema ktk mkutano wa kkkt.Sasa sijui inakuwaje ikiwa viongozi wa dini ambao wanaingia kwa mitego ya faida yao na wala hawajali madhara ya madawa hayo.
3- Serikali itakuwa vizuri kama mtatoa zawadi kwa raia watakao toa ushirikiano kwa kuwakamata mijangili maana ni motisha kwa kazi nzuri.
4- Tunaomba muwataje tu hao wala hatuwezi kuwafanya lolote ni kwa faida ya wananchi pamoja na viongozi wengine wa dini ili waache tamaa.
Siamini hata siku moja, hii ni uzushi mtupu. Kama kuna watu wamekiri kujihusisha na uingizaji wa madawa ya kulevya kwa nini polisi hawaja wakamata? ni kwa nini waachiwe eti tu kwa sababu ni viongozi wa dini? yaani wao wafanye makosa halafu pia wawape masharti polisi wasiwataje majina yao? Tusidanganyane hapa, hizi taarifa hazina usahihi hata kidogo!
ReplyDeleteToka lini viongozi wa kidini wakawa na immune ya kukamatwa na kufunguliwa mashitaka nchini tanzania?
ReplyDeleteHawa watu wamekiri kabisa kujihusisha na uingizaji wa mdawa, tena wamekiri bila ya kulazimishwa, sasa kwa nini polisi wanshindwa kuwafikisha mahakamani? wanataka ushahidi gani zaidi ya huo?
vijana wengi wa kitanzania wamefariki, wamepata wazimu, wana maradhi, wamekuwa majambazi, na wengine wamo mitaani wako addicted na mdawa ambayo watu kama hawa sita (tunaoambiwa wamekiri) wanayaingiza nchini.
Tena inakuwaje leo mkosa ndie anaetowa mashart kwa polisi eti wasitajwe majina yao! why? Watanzania tunakwenda wapi? Kwa mtindo kama huu daima tutakuwa tunachekwa na mataifa mengine.