Mheshimiwa Anna Abdalah,Kiongozi wa msafara wa Kamati Maalumu ya Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,iliyopewa jukumu la kwenda nchini Malaysia,kuchunguza na kubaini uwezo wa Kampuni ya IRIS ya nchini humo,ili kubaini uwezo wa kampuni hiyo kutekeleza jukumu muhimu la kutengeneza vitambulisho vya Kitaifa. Mheshimiwa Anna Abdalla,alisema kuwa watanzania hawana sababu ya kuhofia uwezo wa kampuni hiyo kwani ni kampuni kubwa na ina wataamu na teknolojia ya hali ya juu ya kutengeza vitambulisho ambavyo ni vigumu mno kughushiwa na havichakai haraka.Alisema kuwa Kampuni ya IRIS imetengeza Vitambulisho vya Utaifa kwa nchi mbali mbali  Duniani.
Mbunge wa Maswa Mh. John Shibuda,akizungumza na waandishi wa habari jana mchana,Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam,mara baada ya kuwasili kutoka nchini Malaysia ambako  yeye na wabunge wenzake walikwenda kuchunguza sambamba na kubaini uwezo wa kampuni ya IRIS ya nchini humo iliyopewa zabuni ya kutengeza vitambulisho vya Kitaifa.Shibuda aliishauri serikali kutenga bajeti haraka kwa ajili ya kuanza mradi wa kutengeneza vitambulisho vya Kitaifa.Aliongeza kusema kuwa umuhimu wa  Watanzania kuwa na Vitambulisho vya Kitaifa haukwepeki.
Waheshiwa wabunge wakipata chai Jana asubuhi,mara baada ya kuwasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere,Dar es Salaam,wakitokea nchini Malaysia,ambako  walikwenda kuchunguza sambamba na kubaini uwezo wa kampuni IRIS,iliyoshinda na kupewa zabuni ya kutengeneza vitambulisho vya Kitaifa.
Baadhi ya Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja. Picha  na mdau Victor Makinda

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 12, 2011

    Mhe. Mama Machangu tulikuwa tunacheza nae Bolingo hapa Marekani kwenye hafla moja nyeti sana..kama wiki 4 zilizopita. Dah kweli huyu mama si wa kawaida. Congratulations mama.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 12, 2011

    Na muwasifu tu kwa sasa, hadithi isije ikabadilika hapo baadaye...

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 12, 2011

    Hivi do we need a huge delagation like this to investigate or approve IRIS company? Nauli zao na gharama zingine zingeweza kutumika kununua madawati ya shule watoto wa Kitanzania wanaokaa chini. U need 2 intelligent people to do all this!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 12, 2011

    We unafanya mchezo na posho?

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 13, 2011

    Maoni yangu umeyazika. Mimi nilihoji nanai atakaemtetea matanzania siku itakayogundulika kuna dosari- kama ipo- katika mkataba huu? Wabunge wasijihusishe hivi na kumwaga sifa namana hii. Wametekwa, wamejisahau au vyote? Are they PR or marketing officers for IRIS or are they our representatives? Who will check the executive arm of government when the legislative arm is collaborating with the executive? Wabunge hawa waliyokwenda na kumwaga sifa si moja kwa moja hawataweza kushiriki kwenye kamati ya uchunguzi au kura kuhusu mkataba wa IRIS au ripoti ya mkataba wa IRIS siku ya siku ikitimia?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...