Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai (CCM) akipata maelezo kutoka kwa mtaalamu wa mradi wa Biofueli Bi. Ester Mfugale mara alipotembelea banda la Wizara ya Nishati na Madini kwenye maonyesho yake yanayoendelea kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kambi ya Upinzani Mhe. Freeman Mbowe (CHADEMA) akipata maelezo kutoka kwa mtaalamu wa kampuni ya vifaa vya umeme jua ya Ensol Tanzania Limited inayofadhiliwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Bw. Godwin Msigwa mara alipotembelea banda hilo ili kujionea shughuli zake
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Bw. David Jairo akipata maelezo ikiwa ni pamoja na kuonyeshwa juu ya shughuli za upimaji wa mafuta ya magari unavyofanywa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) mara alipotembelea banda hilo kwenye maonyesho ya Wizara ya Nishati na Madini yanayoendelea kwenye viwanja vya bunge mjini Dodoma. Anayetoa maelezo ni Mhandisi Melania Kamugisha ambaye ni mtaalamu wa mamlaka hiyo
Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Gregory Teu, akipata maelezo kutoka kwa mtaalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Assa Mwakilembe juu ya shughuli zinazofanywa na Wizara hiyo mara alipotembelea banda hilo kwenye maonyesho yake yanayoendelea katika viwanja vya bunge Dodoma.
Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Gregory Teu, akipata maelezo kutoka kwa mtaalamu kutoka kampuni ya Arti Tanzania Limited inayofadhiliwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Bw. Abdalah Seushi juu ya shughuli zinazofanywa na kampuni hiyo mara alipotembelea banda hilo kwenye maonyesho ya Wizara ya Nishati na Madini yanayoendelea katika viwanja vya bunge mjini Dodoma.
Waziri Kivuli wa Wizara ya Nishati na Madini Mhe.John Mnyika (CHADEMA) akimsikiliza kwa makini Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini Nchini (TMAA) Bw. Paul Masanja mara alipotembelea banda hilo ili kupata maelezo juu ya shughuli za ukaguzi wa madini zinazofanywa na Wakala huo.Picha na Greyson Mwase.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 18, 2011

    Mditi makoti hayo Eng mzima?, unazeeka

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...