Wakongwe wakirekodi vibao vyao Metro Studios kwa Allan Mapigo |
Kanku Kelly, Mafumu Bilali na King Maluu |
Timu ya wakongwe wa muziki wa dansi nchini inayowakusanya wanamuziki akiwemo King Kikii, Mafumu Bilali, Bombenga Kasongo Mpinda, John Kitime, Abdul Salvador, Babu Njenje, Waziri Ally, Kanku Kelly, King Maluu, Andy Swebe, Juma Ubao na wengineo, wanatarajia kufanya tamasha lao ambalo hufanyika kila mwaka na safari hii liko njiani kuelekea kileleni kwani linatarajiwa kufanyika kwenye ukumbi wa Selander Bridge Club, maeneo ya Upanga jijini Dar, leo Ijumaa tarehe 22 Julai 2011.
Lengo la tamasha hilo ni kuhuisha uwepo wa wanamuziki wa zamani kwa kudhihirisha kuwa uwezo wao kisanii bado uko juu, halikadhalika mchango wao katika kudumisha sanaa ya muziki wa Tanzania upo pale pale na pia kuikumbusha jamii kuwa walikuwepo, wapo na wataendelea kuwepo.
Nia yao nyingine, ni kuweka daraja baina ya wanamuziki wakongwe na wasasa ili kutengeneza muendelezo mzuri unaotokea kwenye chimbuko la muziki wa kitanzania na kuwaonesha vijana wanaochipukia kisanii kuwa muziki umetoka wapi, unaenda wapi na umefika wapi.
Abdul salvador, Waziri Ally na John Kitime |
Siku hiyo inatarijiwa kuwa ni siku ya aina yake kwani wakongwe hao wanatarajia kutambulisha wimbo wao mmoja na mpya kati ya nyimbo tatu walizorekodi, na wimbo huo unajulikana kwa jina la Tanzania, wakiwa wame urudia katika midundo ya kisasa,kwani wenyewe ulipigwa na Atomic Jazz Band chini ya utunzi wake Steven Hiza mnamo mwaka 1965.
Wakongwe hao wameshakamilisha nyimbo zao tatu ikiwepo hiyo Tanzania, Miaka Hamsini ya uhuru pamoja na Kilimo kwanza na zote hizo chini ya usimamizi wake Prodyuza Allan Mapigo wa Metro Studio.
Kwa kuwapa Saport wakongwe hao ni kuchangia kwa kiasi kikubwa kuuinua muziki wa watanzania.
Wote Mnakaribishwa
Wakongwe Juma Ubao na Andy Swebe mazoezini
Kasongo Mpinda na King Kikiii
Marashi ya Karafuu...
Mbona hamjasema kiingilio itakuwa sh ngapi,,na shoo itaanza sa ngapi?
ReplyDeleteMdau
Dr Ray