Mkuu wa Dawati la Elimu na Mafunzo kwa Umma wa Takukuru Mkoa wa Morogoro, Mercy Manyalika ( aliyesimama mbele) akitoa mada ya wajibu wa walimu katika mapambano dhidi ya Rushwa kwa baadhi ya walimu wanaofundisha somo la uraia kutoka Shule za Sekondari zilizopo Manispaa ya Morogoro.
Mkuu wa Takukuru wa Mkoa wa Morogoro, Stella Mpanju ( wanne kutoka kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya walimu wanaofundisha somo la uraia katika shule za Sekondari zilizipo Manispaa ya Morogoro , ambapo Taasisi hiyo kupitia dawati la elimu na mafunzo kwa umma iliwapatia semina walimu hao kuhusu wajibu wa walimu wa somo hilo katika mapambano dhidi ya Rushwa Shuleni na kwenye jamii nzima.picha na John Nditi.
Huu ni upotezaji wa muda. Sasa unawapa waalimu somo la kupambana na rushwa kwani wao ndo wala rushwa? (akina nanihii) hamuwapi hilo somo mnaona ni vizuri kuwapotezea muda waalimu????????
ReplyDeleteWatz bwana uonevu umekidhiri, walimu walakula rushwa na wapi wanaipatia? Kwanini wasipewe hilo somo bandarini ambapo mizigo yetu inazungushwa ili tutoe chochote? au TRA, Polisi, mahakamani na wafanyakazi wote wa serikali? mbona hata kutokutenda haki ni rushwa tu hata hawa wanaotoa hilo somo nao wanahitaji somo ili wasiwaogope watu kwa vyeo au ukubwa? Waacheni waalimu kwanza waalimu hawatendewi haki Tz vipi wafanyakazi kama bank wanapewa maziwa ya kuwapelekea watoto, chai ofisini ila waalimu hawana na ndo chanzo cha kila mwenye elimu?
ReplyDeleteFikirini tena. Na tunahitaji kuwasikia na kuwaona mkiwafundisha department nilizotaja. Na michuzi please usinibanie hata kama nimechafua hali ya hewa.
hasa rushwa ya ngono.
ReplyDelete