Ndugu wadau, Kwa muda mrefu serikali yetu imekuwa ikisisitiza kuwa ajira ambazo watanzania wana uwezo wa kuzifanya wageni kutoka nje hawaruhusiwi kuzifanya. Msisitizo huu unatokana na malalamiko ya waTanzania katika sekta nyingi kujikuta ajira zao zikichukuliwa na wageni kutoka nje ya nchi yetu tena bila kuwa na kibali cha kufanya kazi.
Zamu hii ni kilio cha Tour Guides wa Kitanzania katika kampuni ya KER & DOWNEY SAFARIES ambao walikuwa wanajipatia riziki yao kubwa kutokana na tip walizokuwa wanapewa na watalii wanao wapeleka kuona vivutio vyetu mbalimbali vya kitalii hasusani mbuga za wanyama.
Kwa muda wa miaka 12, nimekuwa nikifanya kazi kama muongozaji wa wageni katika hifadhi ya ngorongoro, tarangine, Serengeti napia mlimani kilimanjaro. Lakini kwa bahati mbaya nimeachishwa kazi, na wenzangu wengi tu. makampuni mengi ya kitalii kutoka nje yamewaajiri Tour Guides kutoka nje(wazungu wenzao) huku wale wa kitanzania wakibakia kuwa madereva kama unabahati ya kuwa na kazi.
Tour guide hawa wamekuwa wakijichanganya na watalii na kwa sababu wote ni wazungu inakuwa vigumu kugundua kama mmojawapo siyo mtalii bali ni tour guide wa kizungu. Tumelalamika sana kwa sababu hawa tour guide wa kizungu ambao hawajui lolote kuhusu mbuga zetu wamekuwa wakichukua ile tip ambayo ni stahili ya madereva ambao wengi wamesoma tour guide.
Kampuni za kitalii kwa mfano yenye ofisi yake Ngaramtoni mjini Arusha inaongoza kwa kuwa na Tour guide wote wazungu lakini hujichanganya na watalii ili wasijulikane. Madereva wake wamekuwa wakilalamikia hali hiyo ambayo wamesema inawafanya kuwa hohehahe kutokana na tips zao kuchukuliwa na tour guide fake wa kizungu. Kinachosikitisha zaidi ni kwamba hawa wazungu uchwara hawana vibali vya kufanya kazi nchini na hawana ujuzi wowote wa Tour guide na mara nyingi hutumia mgongo wa madereva wa Ki tanzania kufanya hiyo kazi.
Mbaya zaidi kuna wazungu ambao wameanzisha makampuni ya kubeba watalii ambao huishi tu porini na huwa hupokea wageni wanaotumia usafiri wa ndege zinazotuwa ndani ya viwanja vya ndege vilivyoko katika mbuga zetu mbalimbali. Mh. Ezekieli Maige naomba utueleze kama unajua hili na kama unajua basi tujibu sisi watanzania ambao mbuga ni zetu kuwa hawa wazungu wanafanya nini kwenye mbuga zetu?
Inakuwa mgeni kumwelekeza mgeni katika mbuga zetu huku serikali imelala usingizi tu huku wenye rasilimali wakibakia wasindikizaji tu? Mpaka lini waTZ tutabaki tukitazama bila msaada rasilimali zetu ziporwa na wwageni mchana kweupe bila kufaidi hata ile staili ndogo kama tip? Maige naomba usikie kilio cha watanzania wenzako inawezekana Mungu alikupa hiyo nafasi utusaidie kama Yusufu alivyowekwa Misri kuwasaidia ndugu zake. tunaomba urudishe heshima ya nchi maana hawa wazungu wanatuonea na kutuona mama huruma.
Mdau
Tour Guide.


Kuna sehemu kunapwaya kwenye Uhamiaji(mambo ya ndani) na wizara ya kazi.Kuna bahadhi ya wafanyakazi katika Idara hizo siyo "royal" kwa nchi yetu.
ReplyDeleteDavid V
Pole ndugu. Wakati mwingine sisi Watanzania tumebobea kwa kulalamika. Sidhani kuandika hapa kwa Njomba kutasaidia sana. Kwanini wewe na wenzako msichukuwe hatua za kumwona Waziri au Naibu wa Waziri wa Maliasili na Utalii au Viwanda na Biashara huku mkiwa na vielelezo vyote? Wakati mwingine tumekuwa tukilalamika au kueleza haya sehemu zisizostahili hivyo kutopata matokeo stahili. Kulalamika kwenye vijiwe hakusaidii chochote.
ReplyDeleteKila la heri.
ndugu yangu hayo nimadogo katika taifa letu la Tanzania na hawa wahusika wanajuwa nenda kwenye viwanda utakutana nayo hasa hawa wazungu na wahindi,nenda kwa wachina hawa usiseme mpaka kwa wasaidizi wa ndani niwachina.Hakuna waziri anaye wajali watanzania inauma
ReplyDeletehii ilionekana zamani sana , kwa nini serikali ya jamhuri mkuu wa mkoa asichukue hatua za dhiada (najua sio kazi yake )akishirikiana na uhamiaji ili kuwatafuta watu hawa.na nyinyi pia kama raia mna haki ya kuwachomea wenye makampuni haya......huku Zanzibar hatakiwi guide kutoka nje,(ikiwa unatoka bara basi huruhusiwi kuongoza bila ya guide wa hapa)ukibadilisha anuani na kuwa mkaazi wa zenji hapo utakwenda chuoni na kupewa kazi.Pia yapo malalamiko ila sio makubwa ....au undeni chama cha maguide na mtetee haki zenu ,huku tunacho (zatoga),afadhali kinasaidia.mtoa mada niandikie ili tubadilishane mawazo kaka yangu. popoban1@gmail.com
ReplyDeleteWatanzania wanaongoza kwa uvivu east africa na ni watu wa kulalamika kila kukicha.Pia nafikiri tusilalamikie sana wageni wanaofanya kazi Tanzania coz kuna watanzania 100 times wanaofanya ambazo zingeweza kufanywa na wazawa wa nchi husika lakini wananchi wao hawajalalamika kama wanavyolalamika wabongo, je unataka nao wafukuzwe ?
ReplyDeleteKingine ni kuwa wa-tz wengi wetu tu wazembe makazini kazi story baada ya kazi na ndio maana umeconcetrate kwenye tips badala ya kueleza tatizo halisi.Pia wewe mleta mada nadhani elimu yako sio nzuri au uwajibikaji sio mzuri ndio maana wakaona hakuna hasara kwa kampuni hata ikikupoteza. Na baadhi ya watu wa tour wana majigambo ya kijinga , na huwa nashidwa kuelewa kwanini, wakati kazi wanazofanya ni unskilled profession ( just vi-course )
Pia nakushauri utafute kazi nyingine coz maisha sio tours peke yake au unaweza kujiajiri pia kama tips hukuzitia kiberiti.
kweli kabisa kwani ukienda kwao wabaguzi kama nini tena wanatusema vibaya mno mimi nashangaa kwanini wamejaa arusha mimi na kaa nje ya nchi kume jaa ubaguzi mno tena isitoshe sisi wanatuita nyani kwakweli mimi siwapendi wazungu wameoa dada zetu wanawanyayasa mno ma kaka zetu ndio msiseme ninaonea uruma mno. mbona nchi yangu imelala hivo . ukiangalia kenya ni majirani zetu lakini wako mbali sana na hawa mali hasili kama sisi why wanatupita hakika ni aibu tena sana
ReplyDeleteKuhusu suala hili , mambo mawili yanatakiwa kuangaliwa.
ReplyDelete1. Ni kweli uzalendo tanzania haupo hasa kwa serikali kutowajali raia wake.
2. Mtoa hoja mmoja hapo juu amegusia jambo moja la muhimu sana - "uvivu". Hili ni tatizo ambalo linaweza likafanya wazungu wakatae kufanya kai na wazawa. Uvivu huu unasababisha mtu kutokuwa 'serious' na kazi. Kama mnashindwa ku deliver mnatarajia mwenye kampuni aendelee kuwalipa mshahara kwa kazi isiyo na faida?
Pia jaribu kuona kama una communication skills inayokubalika na wageni. Pengine hamuelewani na wageni kwa sababu ya uwezo wenu mdogo wa kuwasiliana nao. Customer care ni sifuri kwa watanzania. Vilevile naungana na mtoa maoni kuwa baadhi ya tour guides wa Tanzania mna majigambo yasiyokuwa na lazima hasa wanaotoka Arusha. Nimekuatana nao mara kwa mara lugha wanazoongea si za kistaarabu. wanajiona kama watu waliofanikiwa sana kimaisha wakati utalii ukifa kwa ujinga wenu hamna mtakachofanya baada ya hapo.