Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na wafanyakazi wa kiwanda cha kusindika samaki cha Geoje kilichopo katika mji wa viwanda wa Geoje nchini Korea ya Kusini Juni 7, 2011 baada ya kukagua shughuli za kiwanda hicho .
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua meli itakayofanya utafiti wa mafuta na Gesi kwenye pwani ya Mtwara na Mafia inayomilikiwa na kampuni ya PETROBAS ya Brazil Julai 7, 2011 . Meli hiyo iliyotengenezwa kwenye bandari ya Geoje nchini Korea ambako Julai 8, 2011 inatarajiwa kuzinduliwa itaweka nanga kwenye bandari ya Mtwara miezi miche ijayo ili kuanza kazi ya utafiti wa mafuta na gesi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)


Asante sana Mr.PM.Haya ndiyo mambo tunayotaka kuyasikia na kuona kinachotakiwa tu hapo Siasa zisiingizwe...basi.(Siyo mara ooh mafuta ni sera yangu...aah mimi ndiyo niliyeianzisha....imo kwenye ilani yetu n.k!!).Uganda wameshayagundua.Mafuta yapo mengi sana ukanda huo.Kuna rafiki zangu wengi serikali imewasomesha Masters za Petroleum Ulaya lakini hawajawahi kuzitumia hizo shahada zao.Serikali iwatafute watasaidia sana hicho kitengo.
ReplyDeleteDavid V
Jamani hayo magorofa yote ni sehemu ya meli? Basi litakuwa meli ambalo halijawahi kutokea sehemu za pwani ya Tanzania. Tunaukaribisha huo uwekezaji lakini chonde chonde wananchi wa Mtwara wawe ndiyo first prioties katika kunufaika na raslimali za uchimbaji mafuta na gesi!
ReplyDeleteMdau
HII MELI NI MALI YA TANZANIA ? TUNA MAKAMPUNI MANGAPI KUTOKA NJE YANAYO TAFUTA MAFUTA TOKEA MIAKA YA TISINI, KWA GHARAMA ZA NANI ? (KUTAFUTA MAFUTA NA GESI NI JAMBO ZURI SANA NA YATATUSAIDIA/NUFAISHA KIUCHUMI) LAKINI MTWARA MAFUTA YAPO HAYATAFUTWI/SIYO YAKUTAFUTA.[HAKUNA ASIYE FAHAMU HILI].
ReplyDeleteJe yakipatikana Watanganyika nao watadai ni mali ya Tanganyika pekee na si ya Muungano kama Wazenji walivyodai? Hili ndilo swali nililonalo kichwani.
ReplyDeletemsitudanganye hiyo meli ni ya abiria bhana
ReplyDeleteJAMANI JAMANI CHONDE CHONDE NA MAFUTA MSISAHAU YALIYOTOKEA IRAQ IRAN LIBYA NA NCHI NYINGINEZO ZINAZOTOA MAFUTA
ReplyDeleteMAFUTA NI BORA YASIPATIKANE HUKO NCHINI KWETU MAANA MAFUTA YANA SHETANI MKUBWA WA VITA
TANZANIA IKIPATIKANA NA MAFUTA BASI MKAE MKAO WA KUGOMBANISHWA NA KUPIGANA VITA YA WENYEWE KWA WENYEWE VITA ITAKAYOSABABISHWA NA MATAIFA MAKUBWA DUNIANI
NCHI NYINGI DUNIANI ZINAZOTOA MAFUTA ZINAKUMBWA NA DIMBWI LA VITA KUTOKANA NA MATAIFA MAKUBWA KUINGIA UROHO WA MAFUTA YA WATU MATOKEO YAKE NA HAPO KWETU TUTAUZIWA SIRAHA NA NYINGINE TUTAPEWA BURE ILI TUCHAPANE WANAUME WACHUKUE MAFUTA NA WATUACHIE MAKABURI
MDAU MWENYE UPEO WA MBALI.
Mh! nji za Urabuni zagombana vita isiyoisha, kisa mafuta chonde chonde Tanzania watoto na wanawake. Hatujazoea hali hiyo jamani tumezoea amani na uhuru wetu.
ReplyDelete