Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na wafanyakazi wa kiwanda cha kusindika samaki cha Geoje kilichopo katika mji wa viwanda wa Geoje nchini Korea ya Kusini Juni 7, 2011 baada ya kukagua shughuli za kiwanda hicho .
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua meli itakayofanya utafiti wa mafuta na Gesi kwenye pwani ya Mtwara na Mafia inayomilikiwa na kampuni ya PETROBAS ya Brazil Julai 7, 2011 . Meli hiyo iliyotengenezwa kwenye bandari ya Geoje nchini Korea ambako Julai 8, 2011 inatarajiwa kuzinduliwa itaweka nanga kwenye bandari ya Mtwara miezi miche ijayo ili kuanza kazi ya utafiti wa mafuta na gesi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 07, 2011

    Asante sana Mr.PM.Haya ndiyo mambo tunayotaka kuyasikia na kuona kinachotakiwa tu hapo Siasa zisiingizwe...basi.(Siyo mara ooh mafuta ni sera yangu...aah mimi ndiyo niliyeianzisha....imo kwenye ilani yetu n.k!!).Uganda wameshayagundua.Mafuta yapo mengi sana ukanda huo.Kuna rafiki zangu wengi serikali imewasomesha Masters za Petroleum Ulaya lakini hawajawahi kuzitumia hizo shahada zao.Serikali iwatafute watasaidia sana hicho kitengo.

    David V

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 07, 2011

    Jamani hayo magorofa yote ni sehemu ya meli? Basi litakuwa meli ambalo halijawahi kutokea sehemu za pwani ya Tanzania. Tunaukaribisha huo uwekezaji lakini chonde chonde wananchi wa Mtwara wawe ndiyo first prioties katika kunufaika na raslimali za uchimbaji mafuta na gesi!

    Mdau

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 08, 2011

    HII MELI NI MALI YA TANZANIA ? TUNA MAKAMPUNI MANGAPI KUTOKA NJE YANAYO TAFUTA MAFUTA TOKEA MIAKA YA TISINI, KWA GHARAMA ZA NANI ? (KUTAFUTA MAFUTA NA GESI NI JAMBO ZURI SANA NA YATATUSAIDIA/NUFAISHA KIUCHUMI) LAKINI MTWARA MAFUTA YAPO HAYATAFUTWI/SIYO YAKUTAFUTA.[HAKUNA ASIYE FAHAMU HILI].

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 08, 2011

    Je yakipatikana Watanganyika nao watadai ni mali ya Tanganyika pekee na si ya Muungano kama Wazenji walivyodai? Hili ndilo swali nililonalo kichwani.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 08, 2011

    msitudanganye hiyo meli ni ya abiria bhana

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 08, 2011

    JAMANI JAMANI CHONDE CHONDE NA MAFUTA MSISAHAU YALIYOTOKEA IRAQ IRAN LIBYA NA NCHI NYINGINEZO ZINAZOTOA MAFUTA

    MAFUTA NI BORA YASIPATIKANE HUKO NCHINI KWETU MAANA MAFUTA YANA SHETANI MKUBWA WA VITA

    TANZANIA IKIPATIKANA NA MAFUTA BASI MKAE MKAO WA KUGOMBANISHWA NA KUPIGANA VITA YA WENYEWE KWA WENYEWE VITA ITAKAYOSABABISHWA NA MATAIFA MAKUBWA DUNIANI

    NCHI NYINGI DUNIANI ZINAZOTOA MAFUTA ZINAKUMBWA NA DIMBWI LA VITA KUTOKANA NA MATAIFA MAKUBWA KUINGIA UROHO WA MAFUTA YA WATU MATOKEO YAKE NA HAPO KWETU TUTAUZIWA SIRAHA NA NYINGINE TUTAPEWA BURE ILI TUCHAPANE WANAUME WACHUKUE MAFUTA NA WATUACHIE MAKABURI

    MDAU MWENYE UPEO WA MBALI.

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 08, 2011

    Mh! nji za Urabuni zagombana vita isiyoisha, kisa mafuta chonde chonde Tanzania watoto na wanawake. Hatujazoea hali hiyo jamani tumezoea amani na uhuru wetu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...