
Design tofauti ya Annaluks

Catwalk ikiendelea


Jestina akifanya vitu vyake

model akionyesha nguo za Anna

mambo ya catwalk yakiendelea

model akiwa mzigoni
estina Akifanyiwa mambo ya make up
wadau waliokuja kumpa sapoti Anna
Anna Lukindo (katikati0 akiwa na Mariam Kilumanga(kulia) pamoja na mamodo wake.
---
Salaam,
URBAN PULSE ikishirikiana na Miss Jestina Blog inakuletea matukio katika picha ya Mtanzania mbunifu wa kimataifa Anna Lukindo
(anaetumia jina la Anna Luks) alipoonyesha mavazi yake ya kibunifu mjini London.
Maonyesho hayo ambayo yalifanyika Ijumaa tarehe 19 Agosti 2011 Chelsea Old Town Hall, King's Road, Chelsea London. SW3 5EE.
Vilevile yalienda sambamba na kusheherekea siku ya Ubinadamu(Humanitarian Day) duniani.
Anna ameonyesha ubunifu wake wa kipekee wa kutumia vitambaa asilia mfano gunia, kamba za katani na nyuzi mbalimbali ambazo anatumia ufundi maalum na kutengeneza vitambaa vyake mwenyewe. Wadau kadhaa kutoka katika nyanja tofauti walijitokeza kwa wingi kumuunga mkono na kuvutiwa zaidi kwa kazi zake.
Maonyesho haya yalitayarishwa na Mdoe ambaye ni Mkurugenzi Wa uchaguzi husika wa wasanii wenye vipaji vya maigizo jijini London. Mbali na shughuli nyingine za kidiplomasia yalikuwepo pia mashindano ya kutafuta mshindi wa Tuzo ya Uso wa mwaka 2012 yaliyoongozwa na mwonyeshaji urembo na mwanamichezo Rachel Christie. Baadaye yalifuatia maonyesho mawili ya mavazi "back to back" yaliyofanywa na wabunifu wawili wa mitindo Anna Lukindo wa Anna Luks na "Adopted Culture" msanifu wa rangi, Nana Antwi.
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana na Anna kwa kutembelea tovuti yake hapo chini
Twitter:@AnnaLukindo
ASANTENI,
URBAN PULSE CREATIVE Akishirikiana na Miss Jestina Blog
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...