kuripoti kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Bw. David Jairo aliyekuwa amesimamishwa kazi kutokana na tuhuma zilizoibuliwa na wabunge juu ya changisho la shilingi milioni 50 kwa taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo ili kufanikishwa upitishwaji wa bajeti ya Wizara hiyo mapema Julai mwaka huu
 Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini wakilisukuma gari lililokuwa limembeba Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Bw. David Jairo mara baada ya kuwasili kwenye ofisi za Wizara hiyo.
 Wafanyakazi kutoka Idara ya Nishati iliyopo chini ya Wizara ya Nishati na Madini wakilisukuma kwa nyuma gari lililokuwa limembeba Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw David Jairo mara baada ya kuwasili kwenye Ofisi za Wizara hiyo mapema leo asubuhi.
 Wafanyakazi wa Wizara ya Nishati na Madini wakimpokea Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. David Jairo kwa shangwe mara baada ya kuwasili kwenye ofisi za Wizara hiyo.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Bw. David Jairo akishukuru Mungu mara baada ya kurejea ofisini kwake ili kuendelea na majukumu yake.
 Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja akiwa amemkumbatia kwa furaha kama moja ya mapokezi Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bw. David Jairo mara baada ya kuripoti katika ofisi za Wizara hiyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari mara baada ya kuripoti ofisini kwake mapema leo asubuhi.
Picha zote na mdau Greyson Mwase

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 26 mpaka sasa

  1. The more victimaization the more poor we become-Culture "I tried"

    ReplyDelete
  2. OMG...Wonders will never cease...
    Tanzania ni zaidi ya uijuavyo ndugu

    ReplyDelete
  3. Haina majoto,Tanzania tambarareeeeeeee, kudadeki,Kama kila kiongozi ni gamba kuanzia rais nani awajibishe mwingine.

    ReplyDelete
  4. kwa mtindo huu maandamano lazima

    ReplyDelete
  5. Mungu wangu! Nchi yetu inaelekea wapi?

    ReplyDelete
  6. GAMBA GUMU

    ReplyDelete
  7. Sasa Chadema haijaingia madarakani hali hii. Ikiingia itabidi itafute wafanyakazi wake itafukuza kila. Spoil system. Karume alijaribu, iangalie Zanzibar ilivyo shaghalabaghala. Mpaka walimu wa shule na madaktari walifukuzwa.

    ReplyDelete
  8. Nini cha mno cha kufanya shangwe najua muda mwingi wa kazi umepotea! Hii inatia mashaka makubwa juu ya suala nzima.

    ReplyDelete
  9. Mnashangilia ulaji hey?Kazi bado haijaisha,ndiyo kwanza imeanza..mtaipata.Halafu michuzi hapo wizarani kuna ufisadi ni noma. ukienda kuomba Prospecting Licence ni kama vile unatafuta balaa. kuna 'geologists' kibao wamerundikana humo kusubiri mlungula ofisini badala ya kwenda field kufanya geological mapping kugundua ni wapi kuna possible mineral occurences(nchi yetu bado haijawa 'explored' vya kutosha) mnasubiri wazungu tu,offcourse mimi napiga kazi nje ya nchi..serikali ikiweka kitengo kizuri cha mineral exploration mimi nitarudi tu.wengine hawajui kabisa hata kushika compass kupima Dip/strike/dip direction,plunges,etc("Office geologists"!!).Nina machungu sana na nyie.

    ReplyDelete
  10. Mmmmmmmmh! Haya tumekubali mzee huna hatia. Yalikuwa ni majungu tu.

    Nipashe la leo limeripoti kuwa jumla zilitumika sh milioni 500 (Milioni mia tano) kupitisha hiyo bajeti. Tanzania kuna wizara ngapi? Kama kila wizara inatumia sh milioni 500 kupitisha bajeti, ni kiasi gani cha fedha kinatumika kila mwaka kupitisha bajeti tu?

    Kwa kweli naipenda sana CCM manake haionei mtu. Kama ni majungu yatapigwa chini na waliotuhumiwa watapeta tu. KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI kwa kuwa na serikali yenye vipaumbele vya maendeleo. Very soon Tanzania will be a developed country.

    ReplyDelete
  11. Bongo tambaraaaaare!

    Kupitisha bajeti tu kunatumia mamilioni. Na kama idara zote zilizoandikiwa barua zingechanga ina maana ni mabilioni yangetumika kwenye wizara moja tu.

    Viongozi wetu jioneeni aibu na mumuogope MUNGU. yAANI KWELI MNATUMIA MABILIONI KUPITISHA BAJETI TU WAKATI TAIFA LIPO GIZANI? SEHEMU NYINGI ZA NCHI HAZINA MAJI YA BOMBA, MUHIMBILI WATU WANAKUFA KWA KUKOSA HUDUMA NZURI. NA MAKELELE YOOTE YALIPOPIGWA NA WAPINZANI KUHUSU MATUMIZI MABAYA BADO HAMJIREKEBISHI? KWA MTINDO HUU MNAIPELEKA NCHI NDIPO SIPO.

    ReplyDelete
  12. HONGERA SANA LUHANJO KWA KUTENDA HAKI HUYO JAMAA ALIONEWA TU. YALIKUWA NI MAJUNGU TU. NA SIJUI NI LINI WATANZANIA TUTAACHA MAJUNGU. HAKUNA UFISADI KATIKA NCHI HII. VIONGOZI WETU NI WAADILIFU SANA NA WANATUMIA SHERIA ZILIZOPO KUFANYA MAAMUZI. NAWASHANGAA HATA HAO WANOLALAMIKIA UDA NA MACHINGA COMPLEX. JAIRO ALICHANGISHA HIZO FEDHA KWA MUJIBU WA SHERIA NA TARATIBU ZA WIZARA.

    CCM OYEEEEEEEE! ETI WABUNGE WANATAKA UCHUNGUZI UFANYIKE. UCHUNGUZI GANI TENA ZAIDI YA HUO ULIOTOA MAAMUZI? LABDA MCHUNGUZE NI WABUNGE WANGAPI WALIHUSIKA KUPITISHA HIYO BAJETI.

    ReplyDelete
  13. I real like my Country.

    ReplyDelete
  14. Hii haijakaa sawa kabisa

    ReplyDelete
  15. WAFANYAKAZI, LUHANJO AMESEMA MSITOE TENA SIRI ZA SERIKALI PALE MNAPOZIBAMBA. HAPO LAZIMA KUNA WENGINE WALIHUSIKA KUUZA SIRI NA LEO MNAMPOKEA KAMA SHUJAA WENU. WABONGO NI WATU WAZURI SANA.

    TUNAOMBA 2015 LUHANJO AGOMBEE "URAISI" WA NJI HII. ANAJUA KUTENDA HAKI SANA. TUNAOMBA LUHANJO AINGILIE PIA MADAI YA UFISADI UDA NA MACHINGA COMPLEX ILI HAKI ITENDEKE.

    ReplyDelete
  16. Kubalini tu kwamba kuchangisha fedha ili bajeti ipite ni kosa. Ila kwa sababu Jairo alitumia taratibu zilizowekwa kisheria, ndio maana kaoneka hana kosa. Kwa hiyo kosa si Jairo bali ni sheria zetu tunazozitunga sisi wenyewe kwa manufaa yetu sisi wenyewe. Tatizo tu ni kwamba sheria hizi zinawanufaisha wachache.

    ReplyDelete
  17. Unafiki mtupu

    ReplyDelete
  18. HIVI HIYO BAJETI INGEKATALIWA NA WABUNGE, HIZO PESA ZINGERUDI? NA WAKATI WA KUANDAA BAJETI NYINGINE ZINGECHANGISHWA TENA ZINGINE?

    ReplyDelete
  19. KUNGELIKUWEPO NA MAKOSA MAWILI HAPO.

    KOSA LA KWANZA: KUCHANGISHA FEDHA ILI BAJETI IPITE

    KOSA LA PILI: JINSI PESA HIZO ZILIVYOTUMIKA.

    CAG KAZI YAKE ILIKUWA KUKAGUA JINSI PESA ZILIVYOTUMIKA. HATA KAMA ZILITUMIKA VIZURI BADO GAIRO ANGEPATIKANA NA HATIA YA KUCHANGISHA FEDHA "ILI BAJETI IPITE" HAPA NDIPO TUNAPOSHINDWA KUELEWA. MILIONI MIA TANO "ILI BAJETI IPITE"!!!!!???????!!!!!!

    KAMA ILIKUWA NI HALALI KUCHANGISHA FEDHA ILI BAJETI IPITE, KWA NINI FEDHA HIZO ZISINGEANDIKWA MOJA KWA MOJA KWENYE VITABU VYA BAJETI ILI KUSIWEPO NA HAJA TENA YA KUCHANGISHANA? INAONEKA NI KOSA NDIO MAANA HAMNA BAJETI ILIYOPITISHWA NA BUNGE KWA AJILI YA KUPITISHA BAJETI.

    ReplyDelete
  20. inawezekana uelewa wangu mdogo ila kwanini sisi wabongo tuna tabia ambazo stimes sizielewi? mfano hapo juu ni sababu zipi zinafanya huyu mheshimiwa apokelewe kama rock star??

    this is not about the victimized but rather about the victims.

    ReplyDelete
  21. Walahi unafiki wetu utatumaliza.

    ReplyDelete
  22. KAZI KWELI KWELI, NCHI HII INAHITAJI KIONGOZI AMBAE NI DICTATOR,TULIKOFIKA KUNATISHA.NASHINDWA KUELEWA HUU USANII WA SERIKALI YETU. MUNGU SAIDIA WATANZANIA WALIO WANYONGE.

    ReplyDelete
  23. KWA KUSOMA KOMENTS ZA WADAU WOTE HAPO JUU, KARIBUNI 99.9 PASENTI WAPO SAKASTIKI NA SIRIKALI YETU, KILA MDAU ANAIONA MZAHA.KUNA MMOJA KASEMA KILA TU NI MBABE, NA MIMI NAONGEZEA KUWA KILA MTU ANAJUA SIRI YA MWENZAKE ANAVYOKULA HIVYO KUNA ILE KITU NISITIRI MIMI NA MIMI NITAKUSITIRI AMA KWA LUGAH YA KIINGEREZA NI -SCRATCH Y BACK I'LL SCRATCH YOURS'. CAG KAHUSIKA NA NINI HAPO BADALA YA HOSEA, KWANZA CAG NI MMBONGO AU TUMECHUKUA EKSIPAT TOKA JIRANI? LIOPO MADARAKANI MUELEWE KUWA WANANCHI TUMECHOSHWA NA INABIDI MBADILIKE MARA MOJA, KWANI SAFARI HII CCM NI BORA KILA MTU AJINYAKULIE CHAKE MAPEMA, KWANI TUTAWAWEKA CHADEMA 2015.PIA MALI ZOTE MLIZOTUIBIA Z I T A R U D I KWA 'WANAINJI', KILA AKAUNTI YA UZWIZI AU AILE OF WAIT AU AILE OF MAN ITAFUNGWA NA PESA ITARUDISHWA KWA WALALA HOI.

    ReplyDelete
  24. WAJINGA NI WAJINGA TU; HATUTAELIMIKA KAMWE; NDIO MAANA TUNADANGANYA NA KANGA NA KOFIA TUNAPIGA KURA KUCHAGUA WATU WASIOMUDU MADARAKA. HAPA; MTU ANAKAA GIZANI ; MAFUTA MGOGORO; UNAMWONA ANASUKUMA GARI LA MTU ALIYEKIUKA TARATIBU ZA MAADILI YA KAZI. UCHAFU MTUPU! WATANZANIA TUFUNGUKE MACHO. UNASUKUMA GARI ILI IWEJE?ULIPEWA SEHEMU YA HIYO MICHANGO?UNAFIKI TU. WAKITOKA HAPO WAKIINGIA KWENYE DALADALA NA VITI VIREFU WANAANZA KUMSEMA; OOH; JAMAA ANAKULA BATA; MAMBO YAKE SAFI; HAGUSWI HATA KASHFA IWE KUBWA NAMNA GANI.HUU UNAFIKI UTAISHA LINE?TUELIMIKE WANANCHI WENZANGU!!!!

    ReplyDelete
  25. JAMANI NASIKIA HUYU MTU(JAIRO) KASIMAMISHWA KAZI TENA NA MR.PRESIDENT KUPISHA UCHUNGUZI UNAOFANYWA NA KAMATI YA BUNGE, YA KWELI HAYA???

    ReplyDelete
  26. dah,ingekuwa kuna uwezo wa kujua kesho?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...