Na Veronica Kazimoto – MAELEZO
DAR ES SALAAM
Mazungumzo bado yanaendelea kati ya Serikali na Muwekezaji aliyejitokeza kununua jengo la Mahakama ya Rufani iliyopo katika makutano ya barabara ya Kivukoni na Ohio jijini Dar es Salaam.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Celina Kombani wakati akijibu hoja mbalimbali za wabunge waliokuwa wakichangia hotuba ya makadirio ya bajeti ya wizara hiyo.
“Kuhusu suala la uuzwaji wa jengo la Mahakama ya Rufani, mazungumzo baina ya Serikali na muwekezaji aliyejitokeza bado yanaendelea hivyo basi napenda kuwatoa hofu waheshimiwa wabunge kuhusiana na suala hili,” amesema waziri Kombani.
Waziri Kombani amefafanua kuwa mazungumzo yanaendelea baina ya muwekezaji na ofisi mbalimbali za Serikali kama ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mahakama ya Rufani,Wizara ya Maliasili na Utalii, Wizara ya Katiba na Sheria na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Aidha, Waziri Kombani amesema muwekezaji aliyejitokeza ameahidi kujenga mahakama ya Rufani yenye hadhi kulingana na umuhimu waka kama mhimili mojawapo wa dola.
Kama muafaka utafikiwa kati ya muwekezaji na Serikali jengo hilo la Mahakama ya Rufani litajengwa maeneo ya mtaa wa Chimala mkabala na barabara ya Taasisi ya Saratani ya Ocean Road.
Hivi karibuni vyombo mbalimbali vya habari vimekuwa vikitoa taarifa kuhusiana na jengo la Mahakama ya Rufani kununuliwa na muwekezaji wa hoteli ya Kempinski na kuwa sehemu ya hoteli hiyo kwa ajili ya maegesho ya magari

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. mzungumzo ya nini???? hawawezi kujenga jengo lenye historia kama hili jamani ...sisi wenyewe tujenge hilo jengo jipya au tutafute mwekezaji ambayo hana masharti yatakayo futa historia yetu...europe, america , china , australia, russia , india ...wanavalue majengo yao yazamani ...what is wrong with us?????
    i msafiri

    ReplyDelete
  2. Muwekezaji kujenga mahakama...hii kichekesho kweli.

    ReplyDelete
  3. Jengo lisivunjew jamani tunahitaji majengo ya kihistoria, kama hili na makao makuu ya jiji la Dar-es- Salaam na majengo mengi ya karibu na ufuko wa Dar. Karibu na stesheni kuu ya reli.Majengo hayo yafanyiwe ukarabati, yabadilishwe tu mabomba ya maji, nyaya za umeme yawekewe vipoza joto basi. Ni heshima ya nchi kuwa na majengo ya zamani. Halafu hili la kutafuta mwekezaji kujenga ofisi ya serikali, tena ofisi nyeti kama mahakama nalo naliona haliko sawa. Tumieni tu kodi zetu, au wizara ya ujenzi kama bado ipo ijenge hiyo mahakama.

    ReplyDelete
  4. It is still a VERY BAD IDEA. How can the government surrender the sovereignty of the county to a hotel chain. The President and his cabinet should be ashamed for not standing up to the dignity and self determination of Tanzania. Next Microsoft or Starbucks will ask for the site of State House to build a coffee house and This Commander in Chief and his cabinet will sell the State House for a price of a few dollars. It is an insult to the heroes who died defending Tanzania when our leaders now surrender our country without even a fight. Someone needs to remind these people TANZANIA IS A RICH COUNRTY AND WE DON'T NEED cheap handouts from an American Hotel chain...

    August 26, 2011 1:22 AM

    ReplyDelete
  5. nimeamini ama kweli pesa ndio kila kitu, ipo siku atakuja fogo atasema naye anataka apewe eneo la ikulu pale magogoni atawajengea mbagala, cjui wanetu watarithi nini? inji hii hakuna kisichoshindikana. thats why I luv so much Tz.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...