Ndugu Michuzi

Asalaam Aleikum

Mimi ni mtumiaji wa mtandao wa Tigo toka enzi za Mobitel na Buzz. Kwa kweli siku hizi Tigo wanaboa naomba unifikishie ujumbe huu kwao. Wamekuwa na message nyingi sana za promotion. Waambie kwamba zinakera na mimi sio mlalamikaji wa kwanza. Niliona mwandishi mmoja wa gazeti la Mwananchi ameandika makala kuhusu hili. Ni kero kubwa.

 Zinakuja nyingi sana, na mbaya zaidi zinakuja mida yote. Usiku wa manane ukiwa umelala. asubuhi unapopambana na foleni kwenda kazini, yaani mida yote. Mimi mpaka imefikia wakati nikisikia message kwenye tigo huwa sisomi muda huo huo, kwa sababu najua ni hizo hizo promotion nisizozihitaji. 

Tigo wanapaswa kufahamu kwamba sio kila mtu yuko interested na hizo bahati nasibu wanazochezesha, message za bure, sijui simu za bure, internet n.k. Wengine tuko kwenye mtandao kupiga na kupokea simu, kutuma na kupokea message tu! Sasa wanapotuma haya ma-message yao kwa watu kama sisi wanakera na kujaza inbox zetu bure.

 Kwa mfano wangu ukiangalia inbox yangu, message hizi kutoka namba 100 ziko nyingi kuliko message za watu ninaowasiliana nao. Naomba Tigo watangaze namna ambayo wateja ambao hawataki hizo message za promotion zao wanaweza kufanya kwenye simu zao ku-block hizo message.

 Bahati mbaya kasimu kangu ni ka tochi, sijui kama kanaweza kuzizuia. Naamini njia bora zaidi wataifanya wenyewe. Mitandao mikubwa kama yahoo na hotmail huwa wanatoa option, kama utapenda promotional emails zao na makampuni yanayo-advertise au la, unachagua mwenyewe. 

Wanapaswa waelewe kwamba hii simu na huduma yao ninayolipia ni ya kwangu binafsi. Mimi nina haki ya kuchagua niwasiliane na nani. Hakuna mwenye haki ya kutumia simu yangu kama anavyotaka. Sio chama fulani na message zao za kampeni wala sio kampuni ya simu na hayo mapromosheni yao. 

Sizitaki message hizi zinanipotezea usingizi zikitumwa usiku. Sizitaki message hizi zinaniharibia concentration ninapofanya mambo yangu. Sizitaki message hizi zinasababisha nichelewe kusoma message za wapendwa wangu kama nilivyoeleza. Pia sizitaki message hizi zinajaza inbox yangu na kupoteza muda wangu kusoma vitu ambavyo havina maana kwangu.

Najua kama una maslahi nao haitapendeza kuwataja hadharani lakini nakuomba sana unifikishie ujumbe kwao. Nimejaribu kupiga namba yao ya customer service ya 100 lakini inapokelewa na mashine haitoi majibu yoyote. Wanasema ukitaka kuongea na mtoa huduma wao upige 0713 800800 lakini niliwahi kusubiri dakika 10 hawakuongea na mimi mpaka nikakata, na sio mara moja. 

Nimepiga pila line nyingine ya 0713 123103 lakini nayo huwa inaita bila kupokelewa. Kwenye website yao hawana email address ambayo ningewaandikia moja kwa moja. 

Hii ndo njia pekee wanaweza wakapata ujumbe. Wengi wamelalamika kwenye magazeti lakini hawasikii. Naomba uwaweke hewani najua wanasoma blog yako. Mbona sipati usumbufu huu kwenye namba yangu za airtel, sina ya Voda sijui huko hali ikoje!

Asante sana

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. yaani hilo ni tatizo hata mimi limenikuta,nimepigiwa simu nikapokea nimesubiri dk kadhaa bila ya majibu sasa nikajiuliza ikiwa mtu andrive au yuko benki na sehemu kwengineko haiwi tafrani hivyo?!hizo msg ndo usiseme ni tabu tupuuu.
    waangalia hao

    ReplyDelete
  2. nakuunga mkono mdau, yaani umegusa pahala pake, tena sasa hivi wamezusha mtindo mbali ya mesage zisizo na maana, kuna namba wanayoitumia 0901901901 hii namba inanikera kupita maelezo haina muda maalum simu inaita unapokea unaanza kusikiliza upuuzi wao sipendi hii tabia nawachukia tigo kwa kulazimisha promotion

    ReplyDelete
  3. NASHUKURU SANA KWA KUWA UJUMBE HUU UMEWEKWA HEWANI.KWA KWELI NI KERO KERO ZA AJABU, TIGO SIO LAZIMA MTULAZIMISHE HIZO PROMOTIONS ZENU NA KUTUWEKEA NYIMBO ZA AJABU AJABU KWENYE SIMU. WEKENI OPTIONS KWA MTU ANAYETAKA ZINAKERA SANA.

    ReplyDelete
  4. mdau naunga mkono hoja, hawa jamaa wa thumni wanakera sana na msg zao!

    ReplyDelete
  5. yani nakuunga mkono 100% coz hizo message zao zinaboa na kukera they should change their ways ama watu watahama

    ReplyDelete
  6. Naungana na wajumbe wote hapo juu TIGO na sms za promotion zinakera sana. Lakini tusisahau vitu rahisi vina gharama zake. alternative..karibuni VODA,Airtel, Zantel na kwingineko. Kwa nini tung'ang'anie Tigo tu wakati kumeshaoza?

    ReplyDelete
  7. Yaani hata sisi tulioko huku ughaibuni, tukiwapigia wapendwa wetu nyumbani lazima waweke nyimbo na hizo promotion zao, do they know how much are we charged per minute? Wanajua mtu una dharura gani wakati unapiga simu? Come on, tigo tumewachoka, huduma zenu mbovu na mnaboa sana..Nilidhani mumebadilika kumbe mambo yaleyale "tafadhali subiri mtu wa kukuhudumia atapokea simu yako" What is this? Customer care?

    ReplyDelete
  8. naungana na mtoa hoja, kwani acha mesaje hata garama zao wamepandisha kisirisiri baada ya kutuchota kwa promosheni uchwara zao, yaani unampigia mtu wa TIGO mwenzako utadhani unapiga nje ya nchi. ila kwa sasa nimehama huu ni mtandao wa kutuibia. mara ya pili wakaniingizia nyimbo eti niliomba wakati sijagosa hata hiyo star, na wakawa wananichaji kila siku.kuomba kutolewa hadi nikaenda kupanga foleni ofisini kwao.NIMEHAMA!!!!!!

    ReplyDelete
  9. wadau yaani hii namba 0901901901 inauzi sana mi kuna cku kidogo nivunje cmu yangu TIGO WANABOA kupita kiac.

    ReplyDelete
  10. Wadau poleni sana. Hivi hakuna 'Telecommunications Regulatory Authority' hapa nchini ambayo ndio inaangalia malalamiko yote ya wateja wa mawasiliano na hivyo wadau kuyafikisha kwao kama TIGO(Mtandao wa bei rahisi) umeshindwa kuchukua hatua za kuzui kero hizo? Kwa wenzetu ughaibun i suala hilo lingeshakuwa historia mpaka sasa kwani ni kweli malalamiko ni mengi, TIGO ingeshakuwa imepigwa faini ya ukweli na wangejirekebisha. Hivyo nadhani muangalie ni nani 'regulator' wa Mobile Phone companies na labda tungeanzia na TCRA ambao nahisi ndio wanao 'regulate' vyombo vya mawasiliano, na mpaka umpate mtu hapo TCRA ambaye atakuelewa maana mtu mwingine atakwambia hawahusiki na masuala hayo hivyo ulie na TIGO.

    ReplyDelete
  11. Tuchukue hatua.....kila mmoja mwenye kuguswa na hali hii mbaya ya kifisadi na ya kupotezeana muda achukue hatua ya KUUHAMA MTANDAO WA TIGO.....haufai, unakera, unaboa, unauhujumu uchumi wetu!

    Ninajua Relationship Officers wa TIGO wataanza kutupa siasa za kujieleza ili kujisafisha. We are not interested... it is too late!

    Pia Voda na Airtel nao wameshaanza ujinga huu! This should be a warning to you as well.

    ReplyDelete
  12. Mimi nafikiri baada ya kumuomba Tigo halafu akaja na mtandao mwingine tuombe tena, inabidi TCRA kama regulator watoe maelekezo maana hizi ni haki za mteja! Mkataba wa mteja na Tigo uko kwenye service sasa hizi free promotion labda waanze kutulipa kwa kuzisikiliza--hapo hata kwa asiyetaka anaweza kujitoa!

    ReplyDelete
  13. WAKUU TATIZO SIO HIZO SMS ZA PROMO TUU, KWA SASA WANAPROMOTION SIJUI YA BAADA YA DAKIKA MBILI NUSU BEI, SASA UKIPIGA SIMU KWANZA HAMUELEWANI THEN KABLA HAIJAFIKA DAKIKA YA PILI INAKATIKA...UNAJIKUTA MTU UNAPIGA SIMU KAMA MARA TATU NDIO UMALIZE MAZUNGUMZO YAKO...MIMI NI MTEJE WA TOGO TOKEA IKIWA MOBITEL ILA KWA HAKIKA KWA SASA NAFIKIRIA KUWAHAMA...NIMEWAPA HADI MWISHO WA MWEZI HUU HALI NI HII HII NATIMKA...

    ReplyDelete
  14. hawa jamaa ni wezi hakuna mfano, yaani mimi hizo msg ndo sitaki hata kuongelea, na hiyo no wanayopiga ndo kero kero,promosheni wezi hakuna mfano, hata ile milioni 100 hakuna aliyeshinda ni changa la macho, wezi wakubwa... mimi sichezagihuo upuuzi wao hata siku moja... kazi kuwaibiawatu na wenye vihela vyao vya ngama..soon nahama acheni wizi

    ReplyDelete
  15. yaaani kwa kweli umetukuna wengi tigo wanaboa ile mbaya bora hata air tell kama hutaki msg inakubali ku stop lakini tigo unaeza kufikiri ni message ya maan kumbe ishu zao za promotion na sasa wamekuja na ujinga mwingine wa kumpigia mteja simu nakuongea sijui tigo chat jamaa ina boa simu mpaka usiku khaa hawa tigo ni wazushi mi naona mwisho ni kuwakukimbiza wateja too much!!!

    ReplyDelete
  16. TCRA mko wapi??????????????????????????????????????

    ReplyDelete
  17. Hameni huko mliko, matatizo ya kujitakia hayo!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...