Meneja Huduma wa Bidhaa za Vodacom, Elihuruma Ngowi akifafanua jambo juu ya huduma ya M Pesa kwa washiriki wa Shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011 katika kambi yao iliyopo jumba la Vodacom jijini Dar es Salaam jana.
Baadhi ya washiriki wa shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, wakijisajili katika huduma ya M Pesa baada ya kupata semina juu ya faida na umuhimu wa kuwa umejisajili katika huduma hiyo jana wakiwa Kambini katika Jumba la Vodacom.
Afisa Utawala wa Huduma ya M Pesa kutoka Vodacom, Emmanuel Pallangyo akigawa viperushi vilivyo na maelezo ya namna huduma ya M Pesa kwa washiriki wa Shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011 katika kambi yao iliyopo jumba la Vodacom jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wa shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, wakipiga picha na mabaunsa waliovalia vazi la M Pesa “Super Man” baada ya warembo hao na wenzao kupata semina juu ya faida na umuhimu wa kuwa umejisajili katika huduma ya M Pesa jana wakiwa Kambini katika Jumba la Vodacom.
Washiriki wa shindano la Vodacom Miss Tanzania 2011, wakipiga picha na mabaunsa waliovalia vazi la M Pesa “Super Man” baada ya warembo hao na wenzao kupata semina juu ya faida na umuhimu wa kuwa umejisajili katika huduma ya M Pesa jana wakiwa Kambini katika Jumba la Vodacom. (Picha na Mpigapicha wetu).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...