Kutokana na maagizo ya wadau wengi kwa Globu ya Jamii kuhusu kurejesha tena Libeneke la TASWIRA ZETU, imetubidi tutii amri hiyo halali bila matatizo.

TASWIRA ZETU ni Libeneke la Globu ya Jamii inayokuletea taswira za aina mbali mbali toka kwa Ankal ama wale wote wenye hobi ya kupiga picha. Libeneke hili linatoa nafasi kwa wadau kuonesha ufundi wao, ama udhaifu wao katika fani ya upigaji picha, inakaribisha mijadala na mafunzo ya upigaji picha, na pia ni jukwaa la hata wale ambao hawajawahi kushika kamera lakini wanapenda mambo ya picha.

Kwa heshima na taadhima tunakukaribisha katika L:ibeneke la TASWIRA ZETU uperuzi ama uchangie picha, mada, maswali, mafunzo na kila kitu kinachohusu picha. Lugha ya Kiswahili inasisitizwa ila si lazima sana hasa kwa wale ambao wanaweza kujieleza zaidi kwa Kiinglishi. Pia kuna vitu kibao katika fani ya picha ambavyo havina jina mbadala kwa Kiswahili. Hivyo jisikie huru kuchangia kwa lugha unayoipatia. Lete picha ama maandiko kupitia issamichuzi@gmail.com

Kutembelea TASWIRA ZETU nenda 
www.michuzi-taswira.blogspot.com
Ama kama vipi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...