NA EVELYN MKOKOI

Imeelezwa kuwa, Serikali ilikuwa ikiagiza madawa ya kilimo miaka ya nyuma kwa lengo ya kukuza sekta hiyo na kuyahifadhi katika maghala kwa muda mrefu na utafiti umeonyesha kuwa yaliisha nguvu na kuweza kuleta madhara kwa mazingira na viumbe hai.

Hayo yameelezwa leo na Kaimu Mkurugenzi wa Habari Elimu na Mawasiliano kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC Dkt Vedast Makota alipokuwa akitoa Elimu kwa wananchi waliotembelea banda la Ofisi ya Makamu wa Rais katika maonyesho ya wakulima yanayoendelea katika viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma.

Dkt Makota alisema, Serikali iliona mapungufu hayo na kwa kushirikiana na Benki ya Dunia iliweza kuunda mradi unaoitwa (ASP) Africa Stockpiles Programmes ambao umeweza kuainisha maeneo yote ya viuatilifu hivyo, kuvikusanya kwa ajili ya kuviteketeza, kutoa elimu kwa wananchi juu ya viuatilifu hivyo pamoja na kuzuia mlundikano wa viatilifu hivyo hapo baadae ikiwa na lengo la kuviteketeza ambapo uteketezaji huo unategemea kufanyika nje ya nchi kutokana na kutokuwepo kwa teknolojia ya kisasa nchini ambayo haitaleta madhara kwa mazingira na viumbe hai.

Kwa upande wake Afisa Misitu kutoka Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Timotheo Mande, ameeleza kuwa, tafiti zinaonyesha kuwa Tanzania ina mifumo Ikolojia kilimo ambayo hubadilishwa na Mabadiliko ya Tabia nchi ambayo pia huweza kubadilisha majira ya mvua hivyo huweza kuleta madhara katika kilimo.

Bw Mande ameongeza kuwa Sekta ya kilimo inatakiwa kufanya utafiti ili kujua ni kwa kiasi gani majira ya mvua hubadilika katika sehemu mbalimbali nchini “Hii itasaidia kuonyesha njia sahihi kwa wakulima kutumia kulingana na mabadiliko hayo.”

Aliongeza kusema kuwa mpaka sasa kuna njia mbili tuu ambazo zimeainishwa kupambana na mabadiliko ta tabia nchi ambazo ni kuhimili mabadiliko ya tabia nchi na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...