Home
Unlabelled
mgambo wa jiji wakamata gari la ubalozi dar es salaam leo!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
MichuziBlogV2Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Nadhani hawa jamaa hawajui wanachofanya hapo. Hiyo ni gari ya Ubalozi kuna sheria ambayo inawalinda hao, wasije wakajiona wanafanya kazi kumbe wanaharibu kazi. Kwa upande wangu hawa jamaa siwahafiki kabisa, wapo kwenye upande wa uonevu sana kuliko ustaharabu
ReplyDeleteWanafanya kazi kwa roho mbaya, wivu na chuki kwa walionacho na wanaotumia nguvu zao kupata mlo wa kila siku. Wao wataishia kunyanyasa tu hawana akili hata kidogo...Siku hizi waajiri wanawapenda sana watu wa aina hii....Hongera mgambo kwa kutumia mabavu bila kutimia akili
ReplyDeleteKwanza kamata baada utajua kama balozi au terrorist!!
ReplyDeleteMimi sijui hata nitumie maneno gani kuwaelezea hawa jamaa ambao hata kuwaita mgambo naona taabu kwa sababu sina hakika kama nchi hii ina mgambo wasiotumia akili katika kufanya kazi zao kama hao jamaa.Nadhani wanafanya kazi kwa chuki tu, nyie "mgambo" acheni chuki kwa watu wenye magari siyo kwamba wameyapata kirahisi kama mnavyodhani wamefanyakazi kwa kutumia akili zao na wengine tumenunua kwa mikopo tu ya benk, sasa hizo chuki na njaa zenu msizimalizie kwa watu wenye magari.
ReplyDeleteNawashauri mliowaajiri hawa watu muwe mnawapa darasa kidogo ili waweze kutumia akili katika kufanya kazi zao na sio kutumia mabavu.YAANI WANATIA KINYAA!!!
Hao jamaa akili zao ni kama nyumbu...'ZINATEGWA ZINARORA' kama sijakosea lugha hiyo ya kiikizu!
ReplyDeleteJamani waelewesheni hao sheria za nchi wanatoka porini wanadhani gari ni gari tu alimradi labda dereva anaweza kutoa cho chote.
ReplyDeleteKwa mfano, miaka kadhaa nyuma tulikwenda kwa official visit kwenye kituo kimoja kwa kutumia gari la UN lenye namba za kidiplomasia. Wakati tunaondoka yule mlinzi ambaye alikuwa ni mgambo alilazimisha afanye sachi kwenye lile gari. Dereva alimwachia na alipomaliza sachi yake alimpa kibano cha nguvu na kumwambia akome kuangalia magari yenye namba za kibalozi mpaka atakapopata kibali maalumu.
Ingekua ni gari la mlalahoi mwenzangu na mie limekamatwa hapo wote mngeona sawa tu lazini kwa kuwa ni la 'ubalozi' ndo inakua nongwa, ila sishangai sana kwa kua ni jadi yetu wabongo kubabaikia wageni, sio sisi tu, tabia hii ipo hadi kwa viongozi wetu wakuu wa nchi.
ReplyDeleteNaamini hilo gari limekamatwa kwasababu limesababisaha uvunjifu wa sheria hapo, sasa labda hao mgambo wao wanafanya kazi yao tu kutokana na maelekezo waliyopewa, wao hawatungi sheria. Sidhani kama ni sahihi kuwafumbia macho hawa wageni kwa kigezo tu cha 'ubalozi' wao, sheria itubane wote.
Waajiri wanawapenda hawahawa. Hawawezi kuwapa shule maana wakiwapa shule watashindwa kuwamiliki....wananchi wenyewe tufanye makakati wa kuwaweka kwenye msitari vinginevyo watawaumiza wake zetu wanaojitafutia riziki
ReplyDeletekwahiyo wewe anony uliyepewa lifti kwenye gari la UN unasherehekea nini?
ReplyDeletebwana ikibidi magari yote yafuate sheria na utaratibu. iweje uegeshe gari sehemu isiostahili kwa kisingizio cha immunity?
mgambo wapo kazini, mbona na nyie mkiwa makazini mnafuata oda za mabosi wenu?
mi nashauri hawa mgambo wangepewa utaratibu wa kazi zao maana kukamata gari la ubalozi ni kuidhalilisha serikali ya Tanzania.Tumeona hata vitu wanavyokamata wanaenda kuvitumia majumbani kwao,Serikali isipokuwa macho wananchi wataanza kuwapatia mkong,oto mpaka waone kazi yao chungu
ReplyDeleteSheria itubane sote. hata ulaya kwenyewe hakuna anae chezea sheria!
ReplyDeletekuwa afisa wa ubalozi haimaanishi kuwa uvunje kanuni za kuishi kwenye nchi ya kigeni, waulizeni maofisa balozi wa tanzania kwenye nchi za kigeni kama wanathubutu kupaki hovyo kwa kuwa ni wa ubalozi, sasa kwa nini mtetee mtu anavunja taratibu kwa sababu ni mtu wa ubalozi! sheria haina mkubwa. mgesema kuwa wanaonewa kuwa hawajapaki vibaya kweli lakini eti sababu gari la ubalozi! aibu hiyo tunajipa wandugu
ReplyDeleteAnonymous wa Tue.30,04:43:00 na 04:17PM 2011,
ReplyDeleteMnaongelea sheria, wakati huo huo mnasema gari iweje gari iegeshwe sehemu isiostahili kwa kisingizio immunity? Umeshajua kama hii gari ata ikamatwe ni kazi bure kwani iko juu ya sheria zote za kuegesha magari. Ndio maana nasema ni vizuri kutumia busara kwa ili kwani ukilikamata unapoteza nguvu ambazo ungetumia kuzuia hualifu mwingine. Sheria iko pale tayari, ya kwamba sheria ya kimataifa hairuhusu kuwanyanyasa mabalozi. Je wewe ungejiasikiaje kama mabalozi wa Kitanzania wa kinyanyaswa ugahibuni?!!. Inabidi tufundishane sheria, sana sana mgambo. Kwa sababu watakapopeleka gari hilo kwa boss wao, boss itabidi aliachie kwani sheria inambana,na mgambo wataona wamezalahulika, na labda kufukuzwa kazi. Sheria za kimataifa zinabana kila mtu na wageni wanafuatilia sheria kuliko WaAfrika. Kwahiyo wa kwetu hatuwezi kubadirisha sheria ili itufaliji tutakapo.
Sheria za kidiplomasia ziko wazi; wanabalozi hawana budi kuheshimu sheria za nchi. Hivyo gari hiyo kushikwa ni sawa. Waende mahakamni wakadai kinga. kinga haidaiwi mbele ya mtekelezaji - askari. Na akifika mahakamani anayo mawili kukubadili adhabu ama kudai kinga na hivyo Waziri wa Mambo ya Nje kuiamua hatua gani ya kuchukua - ama kufukuzwa ama kudai malipo. Balozi zetu zote Uingereza, Marekani na Canada zinalipa faini za makosa ya barabara. Hiyo ndio sheria za wenyeji wetu hivi mgambo hapo wamefanya kazi sahihi. Wanaowabeza ndio wa kubezwa kwa ujinga wao!
ReplyDeleteNjaa inawasumbua,watu hawana elimu na wala hajapelekwa kozi yeyote wanaajiriwa tu!Sasa watakuwaje wastaarabu wakati lugha ya kistaarabu hawaijui na wala hawana busara?Mtu aliyokuwa hajasoma na hana ustaarabu elimu yake ni mabavu na lugha chafu!Hayo makampuni yanayoajiri watu wasiokuwa na elimu na ustaarabu ni lazima kwanza wawapeleke kozi ili wawafundishe jinsi ya kazi hiyo inavyoendeshwa,kabla hawajaanza kazi,Ama sivyo watakuwa wanagombana na watu kila siku na kufikishana mahakamani!
ReplyDelete