Bibi Mawazia Kibwana , mkazi wa Kitongoji cha Kinyenze, Kijiji cha Kipera, Tarafa ya Mlali, Wilaya ya Mvomero, akitoa malalamiko kuhusu kubomolewa choo chake na kuwekwa kwa uzio wa seng’enge na kampuni ya Tanbreed Poultry Limited inayomilikiwa Raia wa kigeni aliyeuziwa eneo kubwa la ardhi na kumega sehemu ya mashamba yao wenye mazao ndani yake na kuziba njia yakwenda mtaa wa Mwanga kama walivyokutwa jana Kijijiji hapo
Baadhi ya Wananchi wa Kitogoji cha Kinyenze, Kijiji cha Kipera, Tarafa ya Mlali, Wilaya ya Mvomero, wakipita pembezoni mwa uzio wa senyeng’e iliowekwa na kampuni ya Tanbreed Poultry Limited inayomilikiwa Raia wa kigeni aliyeuziwa eneo kubwa la ardhi na kumega sehemu ya mashamba yao wenye mazao ndani yake na kuziba njia yakwenda mtaa wa Mwanga kama walivyokutwa jana Kijijiji hapo.
Mkazi wa Kijiji cha Kipera, Tarafa ya Mlali, Wilaya ya Mvomero, Ally Kidunda, akizungumza katika mkutano wa hadhara uliokuwa uzikutanishe pande mbili za wakulima wa kijiji hicho na mzungu anayemiliki kampuni ya Tanbreed Poultry Limited inayodai kununua shamba katika kityongoji cha Kinyenze na kumega sehemu ya mashamba yao wenye mazao ndani yake na kuziba njia ya kwenda mtaa wa Mwanga. (Picha na Mroki Mroki). Kwa habari zaidi Bofya Hapa
Duh! Hata njia pia kauziwa. "No Trespassers" inaingia taratibu!
ReplyDeleteHili suala la ardhi litaifikisha nchi hii mahali pabaya. Serikali imeridhika na kejeli zinazotolewa na raia wa kigeni kwamba tuna ardhi kubwa lakini hatuitumii na hivyo kuamua kuwauzia raia hao ardhi. Ukitaka ujue ardhi ya nchi hii ina wenyewe, jitwalie tu hata ekari moja ambayo unadhani haitumiwi halafu subiri watakaoibuka. Ukweli ni kwamba ardhi ya Tanzania yote ina matumizi. Isipokuwa matuymizi hayo hayajaingizwa kwenye mfumo unaotambulika kisheria. Wanaoitumia wanajua nini wanachokipata kutoka huko. Maisha yao yanategemea hayo matumizi. Ni vizuri serikali ikitaka kuuza ardhi ikawakutanisha wananchi wote wa eneo hilo na kukubaliana nao kwanza.
ReplyDeleteSasa mtu anauziwa mpaka njia, kweli nchi imebaki mifupa.
ReplyDeletehivi ni kwanini siku hizi bongo kuna migogogro ya ardhi na hawa raia wa nje????? hawa watu wa ardhi especially mama Tibaijuka tunaomba aishughulikie haraka manake tukichoka zaidi itakuwa kama Libya
ReplyDeleteHii itakuwa nchi tope
ReplyDeleteYani utafikiri hatuna SERIKALI inauma sana. kwanini wasiuziwe ardhi polini wanakuja kwenye vijiji?
ReplyDelete